Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

SERIKALI KUWATUMIA MAWAKALA KUSAMBAZA PEMBEJEO ZA RUZUKU ZA KILIMO KWA ZUA MALALAMIKO

$
0
0
 Mwenyekiti wa Kamati ya Pembejeo za Kilimo Wilaya ya Njombe ambaye Pia ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba amesema Jumla ya Vocha 78 elfu Zitasambazwa Kwa Kaya 78 Elfu Kwa Mkoa Mzima wa Njombe.
Mmoja wa Wakulima Mkoani Njombe Bwana Donatus Mwamanga[DOSMEZA] Akizungumza na www.gabrielkilamlya.blogspot.com

Na Gabriel Kilamlya Njombe

Wananchi Mkoani Njombe Wamekuwa na mitazamo tofauti juu ya zoezi la  utoaji na Usambazaji pembejeo za kilimo za Ruzuku kwa wakulima Katika  Kuelekea Msimu Mpya wa Kilimo  Ambalo Hufanyika Kila Mwaka na Serikali  Kupitia Mawakala Kwa Madai Kuwa Usambazaji Huo Hauwanufaishi walengwa  kutokana na Baadhi ya Mawakala Wasio Waaminifu kuuza pembejeo kwa 
wananchi wenye uwezo wa Kifedha.

Aidha Zoezi Hilo la Usambazaji Kwa mwaka Jana Limefanyika Kwa Mfumo wa  Kutumia Vikundi Mbalimbali Vya Wakulima Ikiwa Kwa Mkoa wa Njombe Benki  ya Wananchi Njombe NJOCOBA Ndio Iliyopewa Dhamana ya Kusambaza  Pembejeo Hizo Kwa Wakulima.

Pia Kupitia Mfumo Huo Benki ya NJOCOBA Imefanikiwa Kusambaza Pembejeo  Hizo Kwa Wilaya Mbili Pekee za Ludewa na Wanging'ombe  Kutokana na Wakulima Kuwasilisha Maombi Kupitia Vikundi Vyao.

Donatus Mwamanga ni Miongongoni Mwa Wakulima Mkoani Njombe Ambaye  Ameishauri Serikali Kubadili Mfumo wa Kutumia Mawakala Kwa Sababu   mfumo huo unatawaliwa na vitendo vya rushwa na badala yake serikali isimamie zoezi la usambazaji kwa kuwa na bei elekezi kwa nchi nzima.

Pia amesema kama serikali inadhamiria kuwainua wakulima mkoani njombe Inapaswa Itoe Ruzuku kwa mazao yote ya chakula na sio nafaka pekee pamoja na kuwahisha pembejeo kwa wakulima kutokana na uwepo wa ucheleweshaji kila mwaka.

Amesema Suala la Kuwatumia Mawakala Ambao Kila Msimu Wa Kilimo Wamekuwa Wakitupiwa Lawama Kuwapunja Wakulima Limepitwa na Wakati na Kinachotakiwa Serikali Ipunguze Gharama za Pembejeo Hizo Ili Ziuzwe Kwenye Maduka Yote Nchini Kwa
Bei Moja.

Naye Mmoja wa Wakulima wa Kijiji Cha Lusitu Katika Halmashauri ya Mji wa 

Njombe Bwana Anjelo Mgaya Amesema Mfumo wa Ugawaji Pembejeo Hizo Kwa 

Kutumia Mawakala Umekuwa Ukigubikwa na Vitendo Vya Udanganyifu na 

Ulaghai Hatimaye Wananufaika Watu Wachache tena Ambao Si Walengwa.

Kwa Upande Wake Mwenyekiti wa Kamati ya pembejeo wilaya njombe na Mkuu 

wa Wilaya Hiyo Bi.Sarah Dumba Amesema Kwa Msimu Huu Mpya wa Kilimo 

Jumla ya Vocha 78 Elfu Zinatarajiwa Kusambazwa Kwa Wakulima wa Kaya 78 

Elfu kwa mkoa Mzima wa Njombe Huku Akitoa Onyo Kwa Watu Watakaohusika 

na Zoezi Hilo Kufanya Kazi kwa Miongozo Itakayotolewa..

Amesema Katika Wilaya ya Njombe Jumla ya Vocha  16 Elfu Zinatarajiwa 

Kusambazwa Katika Halmashauri Zake Tatu za Mji Makambako,Njombe Mji na 

Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Yenyewe.

Hadi Sasa Baadhi ya Wakulima Hususani wa Mazao ya Viazi, na Mazao Mengine 

Tayari Wameshapanda Mazao Yao Huku Serikali Ikiendelea Kuandaa Utaratibu 

wa Namna ya Kusambaza Vocha Hizo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles