Quantcast
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

WANASIASA WASITUGOMBANISHE WANANCHI

Image may be NSFW.
Clik here to view.
Wagombea UBUNGE Jimbo la Njombe Kusini Kulia ni Edward Mwalongo wa CCM na Kushoto ni Emmanuel Masonga wa CHADEMA Wakutwa Live na KAMERA ya www.gabrielkilamlya.blogspot.com


Kulia ni Mgombea Ubunge Jimbo la Njombe Kusini Kupitia Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Bwana Edward Mwalongo na Kushoto ni Emmanuel Masonga Mgombea Ubunge Jimbo Hilo Kwa Tiketi ya CHADEMA.

Na Gabriel Kilamlya Njombe 

mAONI yA mHARIRI

Katika Pilikapili za Hapa na Pale Wanasiasa Hawa Ambao ni Mahasimu Kwa Vyama Vya Kisiasa na Sio Kimaisha Wamekutwa Wakiwa wanakumbatiana Kuulizana Hali ya Kampeni Kwa Kila Mmoja Wao na Mwisho wa Siku Wakajikuta wananaswa na Kamera ya Mtandao Huu na Kupigwa Picha.

Katika Maongezi Yao Wameonekana Kila Mmoja Akitaka Mwenzie Awe Katibu Wake Mara Baada ya Mmoja Wao Kushinda Kiti Cha Ubunge Jimbo la Njombe Kusini Ambapo Vyama Viwili Vyenye Nguvu Vya CCM na CHADEMA Kupitia Wagombea Wake Hao Hapo Juu Wakiwa Katika Maeneo Yao ya Kujidai Wanapiga Stori Bila Shida.

Aidha Wanasiasa Hao Wakiwa Majukwaani Kila Mmoja Huonekana Kumponda Mwenzio Kutokana na Mifumo ya Vyama Vyao Jambo Ambalo Mwananchi Ambaye Hafahamu Anaweza Jua Kuwa ni Mapambano Makali Kwelikweli na Siasa ni Uadui.

Kitu Kama Hicho Kinasababisha Wapiga Kura Kuwa Njia Panda na Kujikuta Hawafahamu Wafanye Uamuzi Gani na Sahihi.

Hali Hii Imetafsiriwa na Wadau Mbalimbali wa Siasa Kuwa ni Siasa za Karne ya Sasa tofauti na Miaka Kadhaa Iliyopita ambapo Siasa Zilionekana Kama za Ugomvi Muda Wote.

Wamesema Siasa sio Ugomvi wa Kuwagombanisha  Wananchi na Wapiga Kura Kinachotakiwa ni Kila Mmoja Azungumze ya Kwake na Mwisho wa Siku Mwananchi Mwenyewe Amchague Anayemtaka Kulingana na Sera Zake.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276