WAZIRI MKUU PINDA AKUBALI YAISHE MILIMA YA KAMETE.
Aahidi kujenga Barabara ya Lami kutoka Chimala Hadi Matamba Makete.
Milima ya Makete iliyomfanya Waziri Mkuu Pinda kukubali yaishe.![]()
 Tanki la Mradi wa Maji wa Mbela Wilayani Makete.
 Waziri Mkuu Pinda akimtwika Maji aliyoyazindua Jana katika Kijiji cha Mbela Makete utakaohudumia vijiji Vinne kwa Hatua za Awali.
 Wananchi wakifurahia Kuzinduliwa Mradi wao wa Maji wenye thamani ya Zaidi ya Shilingi Milioni 200 makete jana.
 Waziri Mkuu Pinda akiwapungia Mkoni wakazi wa Kata ya Matamba Wilayani Makete.
 Wananchi  wa Kijiji cha Ipelele Makete wakiwa na Pombe ya Ulanzi walipo Msimamisha Waziri Mkuu Jana na Kuomba kusaidiwa Trasfoma ya
Umeme.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda Jana Ameridhia kwenda kujadili na kuipandisha Hadhi Barabara Iilyopo kwenye Mlima Mkali na Kona 57 kutoka Chimala Mkoani Mbeya hadi Matamba Wilayani Makete Mkoani Njombe.
Hatua hiyo Imekuja kufuatia Adha kubwa wanayoipata wakazi wa Wilaya ya Makete kwa kushindwa kunufaika na Fursa za Kiuchumi zilizopo Wilayani Humo kwa Kukosa Barabara itakayowasaidia kupitisha mazao yao licha ya Kuwa Barabara Hiyo ina Urefu wa Kilomita 25 Pekee.
Waziri Mkuu Pinda amesema kuwa kutokana na Wananchi hao kushindwa kupata watalii wa Nje ya Wilaya kutoka Mikoa ya Mbeya Dar es salaam na Nchi Jirani kupitia Barabara Hiyo hivyo kwa Hatua za Awali ni lazima aipandishe hadhi ili iwe ya Mkoa tayari kwa Kujengwa kwa Kiwango Cha Lami.
Dokta Binilith Mahenge ni Mbunge wa Makete ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji amesema kuwa Endapo Barabara Hiyo itajengwa kwa Kiwango cha Lami kama alivyosema Waziri Mkuu itawasaidia wananchi hao Kupata watalii Mbalimbali watakao Ingia katika Hifadhi ya Kitulo Pamoja na Kuufikia kiurahisi Uwanja wa Ndege wa Songwe uliopo Mkoani Mbeya katika Kusafirisha Mazao yao.
Jitihada za Makusudi za Mkuu wa Mkoa wa Njombe na Wilaya ya Makete Kumpitisha Waziri Mkuu Katika Barabara hiyo kujionea Hali ilivyo imeleta Mafanikio japo kwa Maneno ya Ahadi juu ya Ujenzi wa Barabara Hiyo.
Pamoja na Mambo Mengine Waziri Mkuu Mizengo Pinda amezindua Mradi Mkubwa wa Maji wenye Thamani ya Zaidi ya shilingi Milioni Mia Mbili utakaohudumia vijiji vinne kwa hatua ya Awali uliopo kata ya Matamba Wilayani Makete.
Aidha Amewataka wananchi Wilayani Humo kutumia Uzazi wa Mpango ili kupunguza Matumizi Makubwa ya Maji pamoja na Kutunza Miundombinu yake kwani kwa Mujibu wa Takwimu zilizopo Mradi huo utashindwa kukidhi haja ya Ongezeko la Wananchi katika Miaka Ijayo.
Hata Hivyo Waziri Mkuu Mizengo Pinda Ameahidi Kuchangia Shilingi Milioni Kumi katika Kituo Cha Kulelea Watoto Yatima cha Matamba Kinachoendeshwa na Kanisa la Kiinjili la Kirutheli Tanzania Wilayani Makete.
Na Gabriel Kilamlya.