Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

CCM WAZINDUA RASMI KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU

$
0
0

NI ZAIDI YA MAFURIKO JANGWANI LEO,

 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi wa kampeni kwenye viwanja vya Jangwani.
 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha
 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 -2020
 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi mgombea mwenza Samia Suluhu Hassan ilani ya uchaguzi ya CCM kwenye uzinduzi wa kampeni uliofanyika viwanja vya Jangwani.
 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli pamoja na mgombea mwenza Mhe. Samia Suluhu Hassan wakionyesha Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015-2020  katikati ni Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ndiye aliwakabidhi ilani hiyo kwenye uzinduzi wa kampeni za CCM Jangwani.
 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikweteakizungumza baada ya kukabidhi ilani kwa mgombea wa CCM
 Umati wa wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakiwa wamefurika kwa wingi kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM Jangwani.

  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wakazi wa jiji la Dar es salaam waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Jangwani.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye akiwasalimu wakazi wa jiji la Dar es salaam waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni kwenye viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam.
 
DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Jakaya Mrisho Kikwete Amesema Kuwa Kazi Kubwa Iliyofanywa na Chama Cha Mapinduzi CCM Katika Kumpata Mgombea Urais wa Chama Hicho Dokta John Magufuli Ilikuwa ni Kubwa na Inayopaswa Kuungwa Mkono Kwa Nguvu Zote.

Dokta Kikwete Ameyasema Hayo Wakati Akikabidhi Rasmi Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM Kwa Miaka Mitano Ijayo Wakati wa Uzinduzi wa Kampeni za Urais,Ubunge na Udiwani Katika Chama Cha Mapinduzi.

Aidha Dokta Kikwete Amemtaja Dokta Magufuli Kuwa ni Kiongozi wa Mfano Katika Taifa Hili na Kwamba Amekuwa Hana Utani Kwenye Kuleta Mabadiliko Makubwa Ndani Ya Taifa.
 
Akizungumzia Mgombea Mwenza wa CCM Samia Suluhu Hassani Amesema Uadilifu Wake na Uchapakazi Wake Kupitia Bunge Maalumu la Katiba na Kazi Nyingine Anafaa Kuwaongoza Tanzania Kama Makamu wa Rais.

Naye Mgombea Mwenza Samia Suluhu Hassan Amesema Endapo Atakuwa Makamu wa Rais Basi Atahakikisha Anapambana na Changamoto za Wanawake Ikiwa ni Pamoja na Kuboresha Mikopo Kupitia Vikoba Endelevu na Kushughulikia Suala la Maji Ambalo Limekuwa Kikwazo Kwa Akina Mama Nchini.
 
Dokta John Pombe Magufuli ni Mgombea Mteule wa Urais Katika Chama Cha Mapinduzi Ambaye Amesema Pindi Atakapochaguliwa Kuongoza Taifa la Tanzania Kama Rais Atahakikisha Analeta Mapinduzi ya Kweli Ikiwa ni Pamoja na Kupokea Mawazo Mazuri ya Vyama Vya Upinzani na Kuyafanyia Kazi.

Hata Hivyo Amesema Kwa Waliobinafsishiwa Viwanda na Wanashindwa Kuviendeleza Basi Wajiandae Kuvirejesha Serikalini.
 


 Hii ndio CCM
 TOT wakitoa burudani kwenye uzinduzi wa kampeni za CCM jijini Dar es Salaam.

 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(kulia) akiwa pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein kwenye uzinduzi wa kampeni za CCM jijini Dar es Salaam.
 Wasanii wa bongo wakiwa jukwaani.







Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276