Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

WALIOPEWA KADI ZA UANACHAMA CCM MITAANI BAADA YA JULAI 15 MWAKA HUU HAWATORUHUSIWA KUPIGA KURA ZA MAONI AGOSTI MOSI NJOMBE

$
0
0
Katibu wa CCM Mkoa wa Njombe Bwana Hosea Mpagike 
 Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Njombe Alatanga Nyagawa

Na Gabriel Kilamlya Njombe

Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Njombe Kimewataka Wanachama  Wapya Ambao Wamechukua Kadi za Uanachama Baada ya Julai 15 Mwaka Huu Kutojisumbua Kwenda Kwenye Matawi Yao Kupiga Kura  za Maoni Kuwapata Wabunge na Madiwani Watakaopeperusha Bendera ya Chama Hicho Katika Uchaguzi Mkuu.

Kauli Hiyo Imetolewa na Katibu wa CCM Mkoa wa Njombe Bwana Hosea Mpagike Kufuatia Kuwepo Kwa Taarifa za Kusambazwa Kwa  Kadi za Uanachama Hivi Karibuni Baada ya Kuanza Kwa Kampeni  za Kura za Maoni Katika Nafasi ya Diwani na Ubunge.

Mpagike Amesema Kwa Mujibu wa Chama Hicho Anayetoa Kadi Hizo ni Katibu wa Tawi na Si Mtu Mwingine na Hivyo Kama Kuna Mwanachama Amepata Kadi Mitaani Badala ya Viongozi Hao Basi Wajue Kuwa Hakuna Jina Lao Kwenye Ofisi Hizo na Kwamba  Siku ya Kupiga Kura Hapo Kesho Wanatakiwa Kufika na Kadi ya  Uanachama na Kitambulisho cha
Mpiga Kura.

Kwa Upande wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA  Mkoa wa Njombe Kimeelezea Juu ya Mchakato wa Kupiga Kura  Kuwapata Madiwani Watakaopeperusha Bendera ya Chama Hicho Katika Kura za Maoni na Kwamba Zoezi Hilo Litaanza Agosti 7  Mwaka Huu.

Akizungumzia Suala Hilo Katibu wa Chama Hicho Mkoa wa  Njombe Alatanga Nyagawa Amesema Kuwa Ratiba Hiyo Itakwenda  Kuanzia Agosti 7 Hadi 12 Baada ya Kutolewa Kwa Ratiba na  CHADEMA Makao Makuu Jijini Dar es Salaam.

Hata Hivyo Ametoa Wito Kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana  na Rushwa TAKUKURU Kuangazia Katika Vyama Vyote Vya Siasa  Katika Chaguzi Hizo Kutokana na Kuwepo Kwa Mianya ya Rushwa 

Huku Maafisa Hao Kuangazia Zaidi Katika Chama Tawala Pekee.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles