Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

KAMANDA WA POLISI DODOMA AKANUSHA UVUMI WA KIFO CHA ANAYEDAIWA KUPIGWA NA JOB NDUGAI

$
0
0


 
 Mgombea akiwa hoi baada ya  kupingwa fimbo 
.............................................................................................................


Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma Limekanusha Uvumi Unaoenezwa Kwenye Mitandao ya Kijamii Juu ya Kufariki Kwa Joseph Eliaza Chilongani  Anayedaiwa Kupigwa na Job Ndugai Katika Kampeni za Kura za Maoni Ndani ya CCM.

Akikanusha Uvumi Huo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi David Misime Amesema Kuwa Julai 28 Mwaka Huu  majira ya jioni Joseph Chilongani alifika katika kituo cha Polisi Kibaigwa akilalamika kuwa wakati wakiwa kwenye kampeni za kujinadi kwa wanachama kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea ubunge kupitia CCM alishambuliwa kwa fimbo sehemu za kichwani na tumboni na Job Ndugai.

Kamanda Misime amesema mtu huyo aliyejeruhiwa alipewa Fomu ya Matibabu Yaani PF3 na kupelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kongwa kwa uchunguzi wa madaktari na matibabu. Amesema Hadi Sasa Mgombea Huyo Ubunge Katika Jimbo la Kongwa Kupitia Chama

Hicho Amelazwa na anaendelea na matibabu Huku Hali yake Ikitajwa Kuendelea vizuri.

Aidha Kamanda Misime amesema uchunguzi wa malalamiko hayo unafanyiwa kazi kwa kupata  maelezo ya watu walio kuwa kwenye mkutano huo wa kampeni na ukikamilishwa jalada litapelekwa kwa Wakili wa Serikali kwa hatua zaidi za kisheria.

Mganga mfawidhi  anaemtibu  mgombea  huyo Dokta Festo Mapunda amekiri  kumpokea  mgonjwa  huyo na kuwa hadi  sasa anaendelea  vizuri Huku Naye Akikanusha   taarifa  za uongo zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii kuwa mgombea huyo amefariki.

Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo ambaye pia ni mdogo wa Dk.Chilongani, Michael Chilongani, Ndugai alichukua uamuzi huo baada ya mmoja wa wagombea anayeitwa Simon Ngatunga kusema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kuwa na ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma na kuahidi kuwa kama atakuwa mbunge atahakikisha kuwa anaziba mianya yote ya ubadhirifu kauli iliyomkera Job Ndugai.

Ilipofika zamu ya Ndugai kujinadi kwa wanachama wa CCM alimtuhumu Ngatunga kwa kusema uongo na kwamba hakuna ubadhirifu wa aina yoyote ndani ya Halmashauri hiyo.Amesema Ndugai aliposhuka jukwaani alianza kumtafuta Ngatunga ili ampige kwa fimbo ambayo huwa anatembea nayo kwenye kampeni hizo.

Wakati akifanya fujo za kumpiga mgombea huyo, Dk. Chilongani alikuwa anampiga picha kwa kutumia simu yake ya mkononi ambapo Ndugai alipomwona alianza kumshambulia kwa fimbo katika maeneo ya tumboni na kichwani hali iliyomfanya mgombea huyo kupoteza fahamu papo hapo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles