Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

NJOMBE DC YAPATA MILIONI 43 KUKABILIANA NA UKIMWI

$
0
0
 
 Wa Kwanza Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Paulo Malala

Na Gabriel Kilamlya  Njombe

Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Imesema Imelazimika Kuviwezesha Vikundi Vya Watu Wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi yaani [WAVVU] Kwa Kutoa Fedha Kiasi Cha Takribani Shilingi Laki Tano Kwa Kila Kikundi.

Kauli Hiyo Imetolewa na Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ukimwi Katika Halmashauri Hiyo Bwana Shaibu Masasi Baada ya Serikali Kuleta Kiasi Cha Shilingi Milioni 43 Katika Bajeti ya Mwaka Ulioishi Mwezi Juni Mwaka Huu.

Amesema Licha ya Ujio wa Fedha Hizo Lakini Bado Jitihada Zinaendelea Katika Kukabiliana na Janga la Ukimwi Ndani ya Halmashauri Hiyo Kutokana na  Kuwepo Kwa Takwimu Kubwa za

Maambukizi Kwa Asilimia 14.8 Katika Mkoa wa Njombe.

Katika Hatua Nyingine Ameeleza Kuwa Kupitia Fedha Hizo Wanategemea Vikundi Hivyo Vitatumia Vizuri  Kwa Kuanzisha Miradi Mbalimbali ya Ujasiliamali Ili Kuwawezesha Kujikwamua Kiuchumi.

Halmashauri Hiyo Ilitenga na Kuomba Bajeti ya Shilingi Milioni 40 Lakini Serikali Imeleta Kiasi Cha Shilingi Milioni 43 Ambazo Zitasaidia Kupunguza  Changamoto Zilizokuwa Zikijitokeza Katika Vikundi Vya Waathirika Hao.

Ifahamike Kuwa Fedha Hizo Zimechelewa Kuletwa Katika Halmashauri Mbalimbali Hapa Nchini na Kusababisha Kuibuka Kwa Malalamiko Kwa Baadhi ya Wagonjwa Ambao Wengine Tayari Walikata Tamaa ya Kutumia Dawa Kutokana na Umbali wa Kutoka Kituo Kimoja Kwenda Kingine.

Hata Hivyo Amesema Kuletwa Kwa Fedha Hizo Shilingi Milioni 43 Kati ya  Milioni 40 Walizoomba  Zimetokana na Fedha Nyingi za Miradi ya Maendeleo Kushindwa Kuletwa Katika Mwaka wa Fedha Uliopita.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles