Baadhi ya Makatibu kata wa CCM Jimbo la Njombe Kusini Wakimsikiliza Mnec wa Wilaya ya Njombe
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Njombe Bwana Oscar Msigwa Akizungumza na Makatibu Kata wa CCM Jimbo la Njombe Kusini.
Na Gabriel Kilamlya Njombe
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Ccm Wilaya ya Njombe bwana Oscar Msigwa amesema kuwa ushirikiano baina ya Nchi ya Tanzania na China utakwenda kuwanufaisha Wakazi wa Njombe kwa kuahidi kujenga viwanda vitatu vikubwa mkoani Hapa.
MNEC Huyo ameyasema hayo wakati Akizungumza na Makatibu wa chama hicho Ngazi ya kata toka Jimbo la Njombe kusini ambapo Amesema katika ziara yake Nchini China amefanikiwa kuahidiwa ujenzi wa viwanda vya kutengenezea Mabati aina ya msauzi( yenye mgongo mnene).
Aidha amesema mbali na kiwanda hicho lakini pia wameahidi kujenga viwanda cha kuchakata matunda pamoja na kiwanda cha
kutengeneza pikipiki zitakazowasaidia vijana kujikwamua kiuchumi.
Pamoja na mambo mengine amesema kwa sasa Nchi ya China amedhamiria kutoa pikipiki kwa gharama ya shilingi Laki tano za awali ambazo deni linalobaki litalipwa kwa kipindi cha miaka miwili.
Aidha bwana Msigwa ametumia fursa hiyo kutangaza rasmi kuwa mbunge wa Jimbo la Njombe kusini ambaye ni spika wa bunge Bi.Anne Makinda kuwa hatogombea tena ubunge katika jimbo hili na kwamba maandalizi ya kumuweka mgombea mwingine mzuri zianze mara moja.
Amesema kazi kubwa iliyofanywa na spika wa bunge katika Jimbo la Njombe kusini kwa kipindi cha miaka kadhaa iliyopita haipaswi kubezwa kwani kuna maendeleo makubwa yaliyopigwa ukilinganisha sasa na kipindi kilichopita.
Hata hivyo amesema wagombea watakaojitokeza kugombea hawana sababu ya kutoa matusi dhidi ya mgombea wengine na badala yake waonyeshe dira na maono Yao badala ya sera za chuki na matusi.
Mwenyekiti wa Makatibu wa CCM wa Kata za Wilaya ya Njombe Bwana Maxona Nathanael Akizungumza na Makatibu kata Toka Jimbo la Njombe Kusini