Quantcast
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

MAELFU WAMSIKILIZA RAPHAEL LULANDALA MSEMWA AKITANGAZA NIA UBUNGE NJOMBE KUSINI[CHADEMA]

Image may be NSFW.
Clik here to view.
Image may be NSFW.
Clik here to view.
Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Njombe Mwl.Raphael Fakh Lulandala Msemwa Akihutumia Maelefu ya Wakazi wa Njombe Wakati Akitangaza Nia Yake ya Kugombea Ubunge Jimbo la Njombe Kusini Kwa Tiketi ya CHADEMA Leo Image may be NSFW.
Clik here to view.

 Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Njombe Raphael Fakh Lulandala Msemwa Kushoto Akiwa na Katibu Wake Mkoa wa Njombe Alatanga Nyagawa Wakati Akitangaza Nia Yake ya Kugombea Ubunge Jimbo la Njombe Kusini Leo




 Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Njombe Alatanga Nyagawa

 Na Gabriel Kilamlya Njombe

Baada ya Wanachama Wengi wa CHADEMA Mkoani Njombe Kujitiokeza Kutangaza Nia ya Kugombea Ubunge Katika Jimbo la Njombe Kusini Akiwemo Katibu wa Mkoa,Mwenyekiti wa Jimbo Pamoja na Viongozi Wengine Hatimaye Naye Mwenyekiti wa Chama Hicho Mkoa Bwana Raphael Lulandala Msemwa Naye Amejitokeza Jana Kutangaza Nia ya Kugombea Ubunge Katika Jimbo Hilo.

Akitangaza Nia Yake Hiyo Akiwa Katika Viwanja Vya National Housing Bwana Lulandala Amesema Endapo Chama Hicho Kitampitisha na Wananchi Wakamchagua Basi Miongoni Mwa Vipaumbele Vyake Vikubwa Atakavyoanza Navyo ni Kuhakikisha Suala la Kilimo Linapewa Kipaumbele Zaidi.

Lulandala Msemwa Amesema Kuwa Uzalendo wa Dhati na Ushirikiano wa Pamoja Utaweza Kuwasaidia Wakulima Kujikwamua na Umasikini Kwa Kuangalia Namna Nzuri ya
Kupata Pembejeo za Kilimo.

Aidha Amesema Suala la Serikali Kuwadanganya Wananchi Kuwa Sekta ya Elimu Imefanya Vizuri Kupitia Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa Ili Hali Shule Hazina Maabara na Miundombinu Safi Ifike Wakati Watanzania Wakatae Kudanganyika Hivyo.

Pamoja na Mambo Mengine Amesema Kama Kiongozi wa Chama Mkoa Anakubaliana na Kazi Nzuri Inayofanywa na Jeshi la Polisi Licha ya Kupiga Mabomu Wananchi Kwani Katika Uchaguzi Mdogo wa Udiwani Kata ya Njombe Mjini Polisi Hao Walikipigia Kura Chama Cha CHADEMA

Mama Merry Msigwa ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake CHADEMA Kata ya Njombe Mjini Ambaye Amewataka Akina Mama Kutumia Fursa Iliyopo Sasa Katika Kujiunga na Chama Hicho Kutokana na Lawama Nyingi Kuelekezwa Kwa Wanawake Kuwa Wamekuwa Chanzo Cha Kukwamisha Ndoto za Vyama Pinzani Nchini.

Hadi Sasa Jumla ya Watia Nia 9 Ndani ya CHADEMA Jimbo la Njombe Kusini Ndio Waliorejesha Fomu Kwa Mujibu wa Ratiba Kati Ya 11 Waliojitokeza Kuchukua Fomu Hizo za Kuomba Ridhaa ya Chama na Wananchi Katika Kiti Cha Ubunge.









Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles