.Wapiga Picha ya Pamoja Kuaga Rasmi Katika Kikao Cha Mwisho Cha Baraza
.Wasubiri Kikao cha Kuvunja Baraza Hilo.
Madiwani Wakiwa Kwenye Picha ya Pamoja Baada ya Kuhitimisha Kikao Cha Mwisho Cha Kawaida Cha Baraza la Madiwani Katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Leo.![]()


Picha ya Pamoja ya Madiwani Katika Kikao Cha Mwisho Cha Kawaida cha Baraza la Madiwani Wakiweka Kumbukumbu ya Miaka Mitano.
Na Gabiel Kilamlya Njombe
Madiwani wa Kata Mbalimbali Katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Wameitaka Serikali Kufanya Utaratibu wa Kununua Risasi Kwa ajili ya Kukabiliana na Wanyamapori Aina ya Nyani Ambao Wamekuwa Wakishambulia Mazao Shambani.
Kauli Hiyo Wameitoa Leo Katika Kikao Cha Mwisho Cha Kawaida Cha Baraza la Madiwani Ambapo Wamesema Kuwa Mazao Yanayolimwa Katika Kata Mbalimbali Zilizopo Katika Halmashauri Hiyo Yamekuwa Yakishambuliwa na Nyani Hao Ambao Wamekuwa Wakivizia Mazao Hayo.
Aidha Wamesema Kuwa Uhaba wa Chakula Kwa Wakulima Hususani Katika Mwaka Huu Katika Kata ya Idamba Huenda Ikawakuta Wananchi Kutokana na Mazao Yao Mengi Kuliwa na Nyani Hao Ambao Wamekuwa Wakiongezeka Siku Hadi Siku.
Katika Hatua Nyingine Baadhi ya Madiwani Wamesema Licha ya Serikali Kutarajia Kuliingiza Suala Hilo Katika Bajeti Lakini Jamii Yenyewe Inapaswa Kuanza Kujipanga Kwa Kuchangishana Fedha Zitakazowawezesha Kukabiliana na
Wanyama Hao.
Akitolea Ufafanuzi Juu ya Uharibifu Huo Afisa Maliasili Katika Halmashauri Hiyo Bwana Ahmad Maguo Amesema Kuwa Mara Nyingi Halmashauri Hiyo Imekuwa na Utaratibu wa Kutoa Risasi Hizo Kwa Watu Ambao Wanamiliki Silaha Katika Maeneo Husika Ikiwa ni Pamoja na Kuendelea Kupanga Bajeti Kwa ajili ya Kuongeza Risasi Hizo.
Paulo Malala ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Ambaye Amesema Utaribu wa Serikali Umekuwa Ukifanya Ukaguzi wa Risasi Ambazo Zimekuwa Zikitumika Jambo Ambalo Limeonekana Kuchelewesha Upatikanaji wa Risasi Hizo .