Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

MWENYEKITI CHADEMA MKOA WA NJOMBE AREJESHA FOMU UBUNGE JIMBO LA NJOMBE KUSINI

$
0
0
 .Wawili Wapotelea Mitini Kati ya 11 Waliochukua Fomu Hizo
 Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Njombe Bwana  Raphael Fakhi Lulandala Akielekea Kurejesha Fomu ya Kuwania Ubunge Jimbo la Njombe Kusini Leo Asubuhi Katika Ofis za Chama Zilizopo Mjimwema 

 
Mwenyekiti Akirejesha Fomu Baada ya Kujaza




Katibu wa CHADEMA Jimbo la Njombe Kusini Akisaini Kupokea Fomu ya Kuwania Ubunge Jimbo la Njombe Kusini Kwa Mwenyekiti wa CHADEMA  Mkoa wa Njombe Bwana Raphael Lulandala

Na Gabriel Kilamlya Njombe

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mkoa wa Njombe Bwana Raphael Lulandala Leo Amefanikiwa Kurejesha Fomu ya Kugombea Ubunge Katika Jimbo la Njombe Kusini Baada ya Kuijaza.

Akirejesha Fomu Hizo Katika Ofisi Zilizopo Mjimwema Mjini Njombe Bwana Lulandala Amesema Kuwa Amelazimika Kuchukua,Kujaza na Kurejesha Fomu Hiyo Kutokana na Jimbo Hilo Kukosa Kiungo Baina ya Wananchi na Serikali Kwa Muda Mrefu.

Amesema Majukumu ya Kitaifa na Bunge ya Mbunge wa Jimbo Hilo Ambaye ni Spika wa Bunge Bi.Anne Makinda Yamemfanya Kushindwa Kuwakumbuka Wananchi Waliomchagua Kwa Kutofika Kwa Muda Mrefu Kuwaona.

Aidha Bwana Lulandala Ameeleza Kuwa Licha ya Kuwepo na Watia Nia Wengi Ambao Kabla ya Kufunga Zoezi la Kurejesha Fomu Hizo Walikuwa 11 Lakini Anaamini Njombe Inakomaa Kisiasa na Kidemokrasia Kwani Hali Hiyo Inawapa Fursa Wananchi Kumpima Kila Mgombea na
Kumpata Mmoja Atakayekwenda Kuwatumikia Kwa Miaka Mitano.

Kwa Upande Wake Katibu wa CHADEMA Jimbo la Njombe Kusini Bwana Obadia Choga Akizungumza na www.gabrielkilamlya.blogspot.com    Jioni Hii Amesema Kuwa Kati ya Wagombea 11 Waliochukua Fomu Hizo ni Watia Nia 9 Pekee Ndio Waliofanikiwa Kurejesha Fomu Hizo Huku Wawili Wakitokomea Kusikojulikana.

Amesema Kwa Ambao Hawajarejesha Fomu Hizo Watakuwa Wameishia Hapo Kutokana na Muda wake Kuishia Leo Juni 25  Mwaka Huu.



Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles