Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

MADIWANI H/SHAURI NJOMBE WACHARUKA H/MJI NJOMBE KUWAIBIA MAPATO KWENYE MAENEO YAO

$
0
0
 
 Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Shaibu Masasi Akifungua Kikao Cha Baraza la Madiwani Leo
 Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba Akitoa Salamu za Serikali Kwenye Kikao Cha Baraza la Madiwani Katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Leo

 Baadhi ya Wataalamu Katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Wakiwa Kwenye Kikao Cha Mwisho Cha Kawaida Cha Baraza la Madiwani







 Baadhi ya Madiwani wa Kata za Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Wakiimba Wimbo wa Taifa Kwenye Kikao Cha Baraza la Madiwani

 Na Gabriel Kilamlya Njombe

Madiwani wa Kata Mbalimbali Katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Wameitaka Halmashauri Hiyo Kuwahakikishia Upatikanaji wa Fedha za Vijiji Ambazo ni Asilimia 26 Kama Ruzuku Toka Halmashauri Kwenda Vijijini.

Kauli Hiyo Wameitoa Katika Kikao Cha Mwisho Cha Baraza la Madiwani Kilichofanyika Leo Ambapo Wamesema Tangu Muda Mrefu Kumekuwepo na Tabia ya Kutolewa Majibu ya Kuwa Fedha Hizo Zinashughulikiwa Lakini Hadi Sasa Wanaondoka Madarakani Hakuna Fedha Jambo Ambalo Linawapa Shida Namna ya Kwenda Kutoa Majibu Kwa Wananchi Juu ya Fedha Hizo.

Aidha Suala la Wizi wa Mapato Unaodaiwa Kufanywa na Baadhi ya Mawakala Kutoka Katika Halmashauri ya Mji wa Njombe  Ambao Wamekuwa Wakiingia Katika Halmashauri ya
Wilaya Hiyo Limechukua Sura Mpya Baada ya Madiwani Kuitupia Lawama Halmashauri Hiyo Kwa Kushindwa Kudhibiti Suala Hilo.

Wamesema Mbali na Halmashauri Kuahidi Kushughulikia Suala Hilo Chini ya Mkurugenzi Lakini Inapaswa Kufahamu Hadi Sasa ni Kiasi Gani Cha Fedha Kilichoibiwa na Halmashauri ya Mji Njombe Kupitia Mawakala Hao Ambao Wamekuwa Wakidai Wamekuwa Wakiingia Pasipo Kujua Mipaka ya Halmashauri Hizo Mbili.

Mkuu wa wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba amewataka viongozi mbalimbali kujiandaa kikamilifu katika zoezi muhimu la uchaguzi Mkuu utakao fanyika oktoba 25 mwaka huu.

Akizungumza  katika Kikao Hicho  amesema kinachotakiwa ni kwa kila mmoja kujiandaa kikamilifu katika zoezi hilo muhimu Litakalo Leta Taswira Mpya ya Serikali ya Ijayo ya Awamu ya Tano.

Aidha amewataka madiwani  kutumia muda walionao kushiriki katika zoezi la kukimbiza mwenge wa uhuru utakaopokelewa katika shule ya  msingi kipagamo mjini makambako hapo juni 26 mwaka huu.

Awali akifungua mkutano huo makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe bwana Shaibu masasi amewataka maafisa watendaji wa kata kuwasimamia maafisa watendaji wa vijiji katika ukusanyaji Mapato kikamilifu kama malengo yalivyowekwa.

Hata hivyo masasi amesema endapo watendaji hao watafanya vizuri katika ukusanyaji  mapato hayo basi itasaidia kutumia fedha zawafadhili kama za ziada badala ya kuendelea kuwa tegemezi.

Pamoja na Mambo Mengine Amesema Wanapofika mwisho wa mwaka  wa fedha 2014/2015 ambao ulianza mwezi Julai 2014, Halmashauri ya Wilaya ya Njombe ilikadilia kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 18.611 kutoka katika vyanzo vyake vya mapato Ambapo Kutoka vyanzo vya ndani Halmashauri ilikadilia kukusanya bilioni 1.286. 

Hadi Sasa Bado Halmashauri Hiyo Haijafikia Malengo ya Ukusanyaji Mapato Hayo Kwani Halmashauri  imekusanya bilioni 8.458 sawa na asilimia 49.02 ya lengo la kukusanya  Bilioni 18.611 Hadi Sasa ikiwa ni mapato ya ndani,ruzuku kutoka Serikali Kuu, wahisani pamoja na nguvu za wananchi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles