Mtia nia Ubunge Jimbo la Njombe Kusini Kupitia Tiketi ya CHADEMA Bwana Ally Mhagama[Dokta Sagasaga] Akitangaza Rasmi Kugombea Ubunge Jimbo Hilo.
Mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Njombe Kusini Ally Mhagama Akizungumza Wakati Akitia Nia ya Kugombea Ubunge Jimbo la Njombe Kusini Leo.
Katikati ni Mke wa Ally Mhagama Mgombea Ubunge Jimbo la Njombe Kusini[CHADEMA]
Mamia ya Wakazi wakimsikiliza Dokta wa Mafisadi Sagasaga Akitangaza Nia ya Kugombea Ubunge Jimbo la Njombe Kusini Leo
Na Gabriel Kilamlya Njombe
Mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Njombe kusini Ally Mhagama [Dokta Sagasaga]Leo ametangaza rasmi nia yake yautaka kugombea ubunge katika jimbo la Njombe Kusini kupitia tiketi ya chama cha Chadema.
Akitangaza nia yake hiyo bwana Mhagama amesema miongoni mwa vipaumbele atakavyo anza navyo endapo chama na wananchi watamchagua ni kuhakikisha anasimamia na kukomboa Mali ambazo zinamilikiwa na ccm badala ya wananchi.
Amesema suala la fedha nyingi za miradi mbalimbali kutumika zaidi kwenye semina na vikao badala ya kuelekeza kwenye Miradi hiyo litakwenda kukoma mara moja.
Ameeleza kuwa miundombinu mbalimbali kama barabara na madaraja ambayo yamekuwa yakijengwa chini ya kiwango itafika mwisho kutokana na wizi unaofanywa na baadhi ya viongozi wanaogawana fedha za miradi hiyo na
kusababisha miradi kuyumba.
Katika maelezo yake lakini pia amesema vijana wanapaswa kujiunga kwenye vikundi sasa kwani fedha ambazo zimekuwa zikitengwa na serikali lakini zinaliwa na wachache zitakwenda kuwekwa wazi.
Baadhi ya wananchi wamehoji maswali mbalimbali ikiwemo matatizo sugu ambayo Yamekuwa yakishindwa
kipatiwa ufumbuzi kwa miaka mingi ambapo amesema endapo atachaguliwa basi uongozi wake utakuwa wa kudai haki kwa maandamano pindi zinapokosekana.
Idadi ya Wanasiasa Ndani ya Chama Hicho Wanaodaiwa Kutia Nia Ya Kugombea Katika Nafasi Hiyo ya Ubunge Jimbo la Njombe Kusini Inafikia 11 Hadi Sasa Huku Vyama Vingine Navyo Vikiendelea na
Mchakato Huo.