Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

NAIBU KAMISHNA WA POLISI DCP ALLY MLEGE AFARIKI DUNIA

$
0
0

indexMkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu anasikitika kuwataarifu wananchi kuwa aliyekuwa Naibu Kamishna wa Polisi DCP Ally Mlege amefariki dunia usiku wa tarehe 21 juni, 2015 katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam.

Marehemu DCP Mlege, alizaliwa mwaka 1960 wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro. Aidha, alihitimu shule ya msingi mwaka 1976 katika shule ya West Meru mkoani Kilimanjaro na elimu ya sekondari katika shule ya Ifunda mwaka 1980, alihitimu mafunzo ya Jeshi la kujenga taifa (JKT) mwaka 1985 kabla ya kujiunga na Jeshi la Polisi mwaka 1989.

Akiwa katika Jeshi la Polisi marehemu DCP Ally Mlege alishika nyadhifa mbalimbali zikiwemo, kamanda wa kikosi cha
utengenezaji wa magari ya polisi, mkuu wa kitengo cha maendeleo na ugavi makao makuu ya polisi, mkuu wa utawala Kanda Maalum ya Dar es salaam na mpaka umauti unamkuta alikuwa ni mkuu wa kitengo cha kuzuia uhalifu makao makuu ya polisi.

Mazishi ya marehemu DCP Mlege yatafanyika siku ya jumatano tarehe 24 Juni 2015, nyumbani kwao Same mkoani Kilimanjaro kwa heshima zote za kijeshi.

INNAL LILLAH WA INNA ILLAH RAJUUN
Imetolewa na:Advera Bulimba -SSPMsemaji wa Jeshi la Polisi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles