Quantcast
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Article 10


 Baraza la Madiwani likiwa kwenye Kikao chake na kumtaka Mganga Mkuu kuhakikisha anatekeleza Agizo la CHF Haraka iwezekanavyo mwezi Julai.

 Dokta James Ligwa akitolea Ufafanuzi juu ya Kushindwa kukamilisha zoezi hilo hadi sasa na kupelekea Madiwani kumgeukia na kusema hayuko Seriousy.

 Diwani wa Kata ya Kifanya Bwana Gotleab Mng'ong'o akionesha Hasia zake juu ya Uzembe wa Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Dokta James Ligwa kwa Kushindwa Kutekeleza agizo la
Kuhakikisha Wananchi wanajiunga na Mfuko wa Afya Vijijini CHF.

 Diwani wa Kata ya Ramadhani Mheshimiwa Alfred Luvanda akiwa kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani Mji wa Njombe.
 Mkurugenzi  Mpya wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Bwana Isaya Moses asema watendaji watakaofanya kazi kinyume na Utaratibu wafungashe Mabegi yao.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Bwana Edwin Mwanzinga akizungumza kwenye Baraza la Madiwani Jana.

Na Gabriel Kilamlya.

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya mji wa Njombe limemjia juu Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo kwa kushindwa kutekeleza agizo la kuhakikisha Wananchi wanajiunga na Mfuko wa Afya Vijijini CHF Licha ya kuagizwa tangu kikao cha Baraza lililopita.

Hali hiyo imekuja kufuatia Baadhi ya madiwani hao kulalamikia Halmashauri hiyo kushindwa kutekeleza agizo la Baraza lililopita kwa kutengeneza vitambulisho na Risiti za wananchi watakao changia hadi sasa licha ya madiwani hao kufanya kazi ya kuwahamasisha wananchi hao tangu awali.

Majibu ya Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Dokta James Ligwa ya kuwa bado zoezi la kutengeneza Vitambulisho hivyo linaendelea limewafanya madiwani hao kukerwa na majibu hayo na Kumtaka Mkurugenzi kuhakikisha anatekeleza zoezi hilo kwa kushirikiana na Mganga Mkuu

Kutokana na Majibu hayo yamewafanya  Madiwani hao kumjia juu Mganga huyo na kusema kuwa amekuwa akifanya kazi kwa kusuasua na hivyo wamesema katika kipindi cha Mwezi Julai zoezi hilo lifanyiwe kazi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles