Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

LOWASA ASIMAMISHA SHUGHULI KWA SAA KADHAA NJOMBE WAKATI AKIOMBA WADHAMINI

$
0
0
Wakazi wajitokeza Kumsikiliza na Kusimamisha Biashara Zao





 Mwenyekiti wa Vijana CCM Mkoa wa Njombe Bwana Imani Fute Akitoa Taarifa ya Wadhamini Zaidi ya Elfu Kumi Waliojitokeza Kumdhamini Lowasa Mkoani Njombe 
 Lowasa akionesha majina ya wadhamini waliomdhamini Mkoani Njombe baada ya kupokea toka kwa katibu wa CCM Mkoa wa Njombe Cremence Mponji Aliyesimama
 Katibu wa CCM Mkoa wa Njombe Bwana Hosea Mpagike Akimkaribisha Edward Lowasa Ili Awashukuru Wadhamini Wake na Wananchi Mkoani Njombe


 Edward Lowasa Akizungumza na Maelfu ya Wananchi Waliojitokeza Katika Kumdhamini 









Na Gabriel Kilamlya Njombe

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Edward Lowasa Leo Amewasili Mkoani Njombe Kuomba  Wadhamini Katika Mchakato wa Kugombea Nafasi ya Urais Mwezi Oktoba 25 Mwaka Huu.

Akizungumza na Wanachama Waliojitokeza Kumdhamini Mbunge Huyo Pamoja na Wananchi Mbalimbali Mjini Njombe Lowasa Amesema Endapo Watanzania Watamchagua Kuongoza Taifa la Tanzania Hatokubali Kuendelea Kuona Watanzania Wanaendelea Kuwa Masikini Ili Hali Taifa Lina Rasilimali za Kutosha.

Amesema Endapo Atapata Ridhaa Hiyo Basi Ataendesha Nchi Kwa Mchakamchaka  na Kwa Atakayeona Anashindwa Kuendana Naye Basi Anatakiwa Kupisha Mapema Kwa Lengo la Kuwakomboa Watanzania.

Suala la Serikali Kununua Mahindi ya Wakulima Kwa Mkopo Amesema Hataki Kulisikia Tena Endapo Atashinda Katika Uchaguzi Huo na Kwamba Kama Serikali Itakopa Mazao Hayo Kwa Wakulima Basi Walipwa na Riba.

Imani Fute ni Mwenyekiti wa Vijana CCM Mkoa wa Njombe Ambaye Amesema Katika Mkoa wa Njombe Zaidi  ya Wanachama Elfu Kumi Wamejitokeza Kumdhamini Lowasa Katika Kinyang'anyiro Hicho.

Kwa Mujibu wa Katibu wa CCM Wilaya ya Njombe Bwana Clemence Mponji Amesema Hadi Sasa Jumla ya Watia Nia 11 Katika Nafasi ya Urais  Ndio Waliofika Kuomba Wadhamini Katika Mkoa wa Njombe.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles