
Mshukiwa Dylan Roof mwenye umri wa miaka 21,Amefikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani kupitia teknolojia ya video.
Polisi Wameyachukulia mauaji hayo katika kanisa la Emanuel AME siku ya jumatano usiku katika mji wa kusini mwa Carolina kama uhalifu wa chuki.
Amekamatwa siku iliofuata yapata maili 200 kutoka mji wa Carolina kaskazini kabla ya kusafirishwa na kurudishwa mjini Charleston.
Gavana wa jimbo la Carolina Kusini Nikki Haley amesema kuwa Roof anapaswa kupewa adhabu ya kifo.