Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

MWENYEKITI WA CHADEMA JIMBO LA NJOMBE KUSINI ALLY MHAGAMA [DOKTA SAGASAGA] KUTANGAZA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE JUMA PILI HII

$
0
0
Mwenye Mtandio mwekundu ni mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Njombe Kusini  Bwana Ally Mhagama Ambaye Anatarajia Kutangaza Nia ya Kugombea ubunge jimbo Hilo Siku ya Juma Pili ya Wiki Hii.
 
Na Gabriel Kilamlya Njombe'
 
Wakati Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Njombe Alatanga Nyagawa Akitangaza Nia Yake ya Kutaka Kugombea Ubunge Katika Jimbo la Njombe Kusini Juni 14 Mwaka Huu,Naye Mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo Hilo Bwana Ally Mhagama Amesema Anatarajia Kutangaza Nia Yake ya Kugombea Ubunge Katika Jimbo Hilo.

Akizungumza na Kituo Hiki Kufuatia Kuwepo Kwa Minong'ono ya Baadhi ya  Wananchi Juu yake Kujitokeza Kuchukua Fomu Kimya Kimya Bwana Mhagama Amesema  Siku ya Juma Pili Atakwenda Kutanga Rasmi Nia Yake ya Kugombea Ubunge.

Aidha Amesema Licha ya Wagombea Wote 12 Ndani ya Chama Hicho Kujitokeza Kutia Nia Lakini Anaamini Yeye ni Chaguo Sahihi Kutokana na Mahitaji ya Wananchi.

Amesema Pamoja na Mambo Mengine Anapongeza Hatua ya Akina Mama Kujitokeza  Kutia Nia Hususani Viti Maalumu Ambao Wameonesha Ujasili Kutokana na Hofu ya Wanawake Waliowengi Kujitokeza Katika Vinyang'anyiro Hivyo.

Katika Hatua Nyingine Bwana Mhagama Amesema Endapo Chama Kitampitisha na Wananchi Wakamchagua Kuwa Mbunge Wao Itakuwa Rahisi Kutoa Kauli Ndani ya Halmashauri na Jimbo  Tofauti na Sasa Akiwa Mwenyekiti wa Chama Pekee.

Zoezi la Watia Nia Kuendelea Kujitokeza Kutoka Vyama Mbalimbali Vya Siasa  Limeendelea Kushika Kasi Katika Maeneo Mbalimbali Hapa Nchini Ambapo Katika  Nafasi ya Urais Kupitia Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi ccm Wanafikia  Takribani Watia Nia 36 Hadi Sasa.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles