Hawa ni baadhi ya Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe wakiwa kwenye Moja ya Vikao vyao kabla ya Kuvunjwa kwa Baraza Hilo June 28 mwaka Huu.
Halmashauri ya Wilaya ya Njombe inatarajia kuvunja Baraza la Madiwani June 28 mwaka Huu kufuatia serikali kutangaza kuanzishwa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe Ifikapo Julai Mosi Mwaka Huu.
Akizungumza na www.gabrielkilamlya.blogspot.com Ofisini kwake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Ya
Njombe bwana Paulo Malala amesema kuwa kutokana Wilaya ya Wanging'ombe kuanzisha Halmashauri yake ifikapo julai Mosi mwaka Huu hivyo ni lazima baraza la Halmashauri Mama livunjwe ili kuwapa fursa ya kuunda Baraza Jipya katika Halmashauri ya Wanging'ombe.
Bwana Malala ameeleza kuwa hadi sasa maandalizi ya kuanzishwa kwa Halmashauri hiyo yanaendelea vizuri kwani tayari Shule ya Msingi Igwachanya ya zamani itatumika kama ofisi za Halmashauri hiyo kwa hatua za Awali wakati ujenzi ukiendelea.
Aidha amesema kuwa mara baada ya kuvunjwa kwa baraza hilo hatua ya uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Hiyo pamoja na Makamu wenyeviti utaendelea kwani kwa mujibu wa taratibu Halmashauri zote zinatakiwa kuwachagua makamu wengine kila Mwaka.