Na Gabriel Kilamlya Njombe
Katibu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mkoa wa Njombe Bwana Alatanga Nyagawa Ametangaza Rasmi Nia Yake ya Kutaka Kugombea Ubunge Katika Jimbo la Njombe Kusini Kupitia Tiketi ya Chama Hicho.
Akizungumza na Vyombo Vya Habari Mara Baada ya Kutangaza Nia Yake Hiyo Alatanga Amesema Endapo Wakazi wa Njombe Watamchagua Kuwa Mbunge Ndani ya Jimbo Hilo Basi Atatumia Uwezo wa Kiushawishi Alionao Katika Kuhakikisha Anawapata Wawekezaji wa Kuwekeza Katika Sekta Mbalimbali Mkoani Njombe.
Alatanga Amesema Tatizo la Soko Kwa Wakulima wa Chai Ndani ya Mkoa wa Njombe Linashindwa
Kupatiwa Ufumbuzi Kutokana na Usimamizi Dini wa Viongozi Waliopo Madarakani na
Kusababisha Adha Kubwa Kwa Wakulima.
Aidha Amesema Ridhaa ya Wananchi Kumchagua Kuwa Kiongozi Katika Uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba
Mwaka Huuu Endapo Chama Kitampitisha Basi Atahakikisha Anawatafuta Wawekezaji wa Nje na Ndani
Ambao Watakuja Kujenga Viwanda Vya Kutosha Vya Chai Mkoani Hapa.
Akizugumzia Suala Sugu la Maji Katika Mji wa Njombe na Maeneo Mengine Hapa Nchini Alatanga
Amesema Uzembe wa Baadhi ya Viongozi Waliopo Madarakani Ndio Chanzo Kikubwa Kinachokwamisha
Kupatikana Kwa Maji ya Uhakika Katika Maeneo Mbalimbali.
Pamoja na Mambo Mengine Lakini Pia Amesema Suala la Ajira Kwa Vijana Litapewa Kipaumbele Zaidi
Endapo Atachaguliwa Kwa Kuwaunganisha Pamoja na Kubuni Mambo ya Kufanya Badala ya Kubaki Bila
Kazi Yoyote.