Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Jackson Saitabau Akifungua Kikao Cha Kujadili Mapambano Dhidi ya Ukimwi Katika Ukumbi wa Mid Town Mjini Makambako Leo.![]()
Baadhi ya Wadau wa Mapambano Dhidi ya Ukimwi Mkoani Njombe Wakiwa Katika Mkutano Mjini Makambako Leo.Watu Wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi Wakiwa Kwenye Picha ya Pamoja na Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Bwana Jackson Saitabau
Viongozi wa Dini Mkoani Njombe Wakiwa Kwenye Picha ya Pamoja na Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Bwana Jackson Saitabau
Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Jackson Saitabau Akiwa Kwenye Picha ya Pamoja na Waratibu wa Ukimwi toka Katika Halmashauri za Mkoa wa Njombe
Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Jackson Saitabau Akiwa na Sekretarieti ya Mkoa wa Njombe Pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la WAVVU(aliyekaa Kulia)
Na Gabriel Kilamlya MAKAMBAKO-NJOMBE
Serikali Mkoani Njombe Imewaomba Wadau Mbalimbali wa Kupambana na UKIMWI Kuangalia Namna ya Kutafuta Fedha Zitakazoendeleza Mapambano Hayo Kutokana na Wafadhili Wengi Kuendelea Kujitoa Siku Hadi Siku.
Kauli Hiyo Imetolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Bwana Jackson Saitabau Wakati Akifungua Mkutano wa Wadau wa Mapambano Dhidi ya Ukimwi Kilichofanyika Mjini Makambako Mkoani Njombe.
Saitabau Amesema Kuwa Kinachotakiwa ni Kwa Kila Mmoja Kuhakikisha Anaendeleza Mapambano Hayo Huku Akiagiza Wadau Katika Kikao Hicho Wanawasilisha Mpango Wao wa Namna ya Kuendeleza Mapambano Hayo Ikiwa ni Pamoja na Mbinu Zilizotumika Katika Kukabiliana na Janga Hilo.
Kwa Upande Wake Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi Bwana Justine Mwinuka Ametumia Fursa Hiyo Kuiomba Serikali Kuhakikisha Inaongeza Kasi ya Usambazaji Dawa za Kufubaza Makali ya Virusi Vya Ukimwi Katika Vituo Vinavyohusika Ikiwa ni Pamoja na Kuongeza Vituo Hivyo Kutokana na Idadi Kubwa ya
Waathirika Kukata Tamaa ya Kutumia Dawa Kutokana na Umbali.
Amesema Kama Baraza Pia Limekuwa Likiwasaidia Waathirika Kuendelea Kuwasilisha Changamoto Zao Ngazi za Halmashauri Ili Ziendelee Kushughulikiwa Kupitia Serikali Kuu na Serikali za Mitaa.
Kwa Upade Wao Washiriki Katika Mkutano Huo Wameitaka Serikali Kuongeza Ujuzi wa Kutoa Elimu Kwa Makundi Mbalimbali Juu ya Masuala ya Ukimwi Wakiwemo Madereva wa Magari Makubwa na Madogo Ambao Wamekuwa Vigumu Kuwafikia Katika Kazi Zao Ikiwa ni Pamoja na Kuongeza Kasi ya Usambazaji Kondomu Kwenye Nyumba za Kulala Wageni.
Dokta Godfrey Balabona ni Mwakilishi wa Mratibu wa Ukimwi Mkoa wa Njombe Ambaye Amesema Hadi Sasa Mkoa Una Jumla ya Vituo 49 Vya Kutolea Dawa za Kufubaza Makali ya Virusi Vya Ukimwi Licha ya Kuwa Bado Changamoto ni Kubwa Katika Mapambano Dhidi ya Ukimwi.
Baadhi ya Washiriki Katika Mkutano Huo wa Masuala ya Ukimwi
Mwenyekiti wa Baraza la Watu Wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi Tanzania Bwana Justine Mwinuka Akionesha Kitabu Cha Muongozo Juu ya Masuala ya Ukimwi.
Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Jackson Saitabau Akihojiwa na Wanahabari Juu ya Hali ya Mapambano Dhidi ya Ukimwi.
Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Jackson Saitabau Akiwa na Wadau Toka Asasi za Kiraia