Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

SHIRIKA LA CUAMM LA KABIDHI VITENDEA KAZI KWA WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII WILAYA YA NJOMBE

$
0
0
 MKUU WA WILAYA  YA NJOMBE AKIZINDUA VITENDEA KAZI HIVYO  ZIKIWEMO BAISKELI



 HUYU NI MUHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII KUTOKA MATIGANJORA




Hizi ni baadhi tu ya baiskeli za Kutembelea Kati ya Baiskeli 50 zilizotolewa.

Na Michael Ngilangwa-Njombe


Mkuu Wilaya Ya Njombe Bi.Sarah Dumba Amezindua Vitendea Kazi 150 Mbalimbali Vya Wahudumu Wa Afya Ngazi Ya Jamii Kwaajili Ya Kuwatembelea Wanawake Wajawazito Na Watoto  Walioko Katika Halmashauri Ya Wilaya Ya Njombe.

Miongozi Mwa Vitendea Kazi Vilivyozinduliwa Na Mkuu Wa Wilaya Ya Njombe Bi.Sarah Dumba Ni Pamoja Na Baiskeli 50,Makoti Ya Mvua 50 Na Gam Buti 50 Ambavyo Vimekabidhiwa Kwa Wahudumu Wa Afya Ngazi Ya Jamii Wa Kutoka Vijiji 25 Vya Wilaya Ya Njombe Ili Kuwawezesha Kuwafikia Kwa Wakati Watoto Na Akina Mama Wajawazito.

Akizungumza Kabla Ya Kuzindua Vitendea Kazi Hivyo Bi.  Dumba Amekemea Tabia Ya Baadhi Ya Watu Ambao Wamekuwa Wakipatiwa Msaada Wa Vyombo Vya Usafiri Kwaajili Ya Kuyafikia Maeneo Ya Utoaji Wa Huduma  Lakini Wao Wamekuwa Wakiuza  Na Kutaka Watunze Na Kuvitumia Kwa Umakini.

Awali Akimkaribisha Mgeni Rasmi Kaimu Mkurugenzi Wa Halamashauri Ya Wilaya Ya Njombe Bwana Abraham Kaaya Ameshukuru Shirika Hilo Kwa Jitihada Ambazo Limekuwa Likifanya Na Kwamba Shughuli Zinazofanywa Na Shirika Hilo Ilitakiwa Zifanywe Na Wataalamu Wa Halamashauri Lakini Anapongeza Kwa Jitihada Zinazoendelea Na Kusaidia Kutatua Changamoto Za Wananchi Wa Wilaya Hiyo.

Akisoma Risala Fupi Mbele Ya Mgeni Rasmi Afisa Mkuu Wa Maendeleo Ya Jumuiya  Kutoka Shirika Lisilo La Kiserikali La CUAMM bI. Neema Lazaro Amesema Kuwa Umbali Wa Baadhi Ya Vitongoji Katika Vijiji  Vinasababisha Wahudumu Kushindwa Kuyafikia Maeneo Hayo Huku Shirika Hilo Likiwa Limefanikiwa Kutoa Mafunzo Ya Wiki Tatu Mfululizo  Kwa Wajawazito 58 .

Aidha Bi. Lazaro Amesema Kuwa  Hadi Sasa Halmashauri Ya Wilaya Ya Njombe Ina Jumla Ya Wataalamu 78 Wenye Elimu Ya Huduma Jumuishi Ya Afya Ya Mama Na Mtoto Mchanga Na Mtoto Chini Ya Umri Wa Miaka Mitano Waliowezeshwa Na Shirika La CUAMM.

Kwa Upande Wake Baadhi Ya Wahudumu Wa Afya Ngazi Ya  Jamii  Wameshukuru Kwa Kupatiwa Msaada Huo  Na Kuahidi Kuyafikia Maeneo Mbalimbali Ambayo Yalikuwa Hayafikiwi Na Wahudumu Wa Afya Hao Ili Kutoa Elimu Ya Mama Na Mtoto Namna Ya Kujifungua Na Huduma Za Kiafya Baada Ya Kumzaa Mtoto.

Vitendea Kazi Hivyo Vilivyozinduliwa Na Mkuu Wa Wilaya Ya Njombe Hapo Jana  Vimeandaliwa Na Shirika Lisilo La Kiserikali La CUAMM  Ambapo Lilianzishwa Mwaka Jana Kwa Mkoa Wa Njombe Na Kuanza Kutekeleza Majukumu Yake Kwa Halmashauri Za Wilaya Mbili Wilaya Ya Njombe Na Makete.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles