Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

MWENYEKITI BAVICHA KIJIJI CHA LUANA AWATAKA WANANCHI LUDEWA KUTOMPOTEZA FILIKUNJOMBE

$
0
0
mbunge  wa  jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe  akizungumza na   baadhi ya  wananchi  wa kijiji  cha Luana waliojitokeza kuungana nae katika maendeleo ya  kuchimba mifereji ya kutolea maji katika barabara yenye urefu wa km 2  aliyowachongea
mbunge  wa Ludewa Deo Filikunjombe  akielekea  kujumuika na  wananchi wake wa  kijiji  cha Luana  kuchimba mifereji ya kutolea maji katika barabara ya kijiji  cha Luana ambayo ameshirikiana na  wananchi hao kuichonga
Wananchi  wa Luana  wakielekea kazini pamoja na mbunge  wao
Wananchi  wa Luana  wazee na vijana  wakishiriki maendeleo na mbunge  wao
Wananchi  wa Luana  wakiwajibika kuchimba barabara
Na MatukiodaimaBLOG 
 
MWENYEKITI wa baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA)
kijiji cha Luana  wilaya ya  Ludewa mkoani Njombe Bw Kalolo Nkwera
amempongeza mbunge wa  jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe (CCM) kwa
jitihada  zake  za uboreshaji  wa barabara za wilaya ya Ludewa  ikiwemo
barabara ya  kijiji hicho yenye urefu wa kilomita 2
 aliyoichonga mbunge  huyo kwa kushirikiana na  wanakijiji kwa gharama  ya  zaidi ya Tsh milioni 54.
Bw 
Nkwera  alisema  kuwa  jitihada zilizofanywa na  mbunge Filikunjombe
katika  wilaya ya Ludewa ni  kubwa na kila mwananchi  wa Ludewa na
wasio  wa Ludewa ambao  wanafika  wilayani  humo ni mashahidi wa
maendeleo ya  sasa  ya  wilaya hiyo na  wao kama  wapinzani wanatambua
mchango mkubwa wa mbunge  huyo katika maendeleo hivyo hawana  sababu ya
kutafuta mbunge zaidi nje ya Filikunjombe.
 
Mwenyekiti
huyo  wa BAVICHA alisema toa kauli  hiyo leo   wakati  akizungumza na
wanahabari  baada ya kushirikiana  na mbunge  huyo na wananchi  wengine
katika shughuli  ya  kimaendeleo ya kuchimba mifereji  ya kupitisha
maji kweye barabara   hiyo mpya .
 

mimi hapa  na  baadhi ya  wananchi  hapo  ambao  wamekuja  kushirikiana
na mbunge Filikunjombe katika uchimbaji wa mifereji  ya  kupitisha maji
katika barabara  hii ni watu  wa  upinzani kama  mimi ni mwenyekiti wa
BAVICHA katika  kijiji hiki ila katika masuala ya  kimaendeleo mambo ya
itikadi  za  vyama tunaweka kando na  kufanya maendeleo …….hii
barabara tunapita  wote hivyo  hatuwezi kuwa  wapinzani wa maendeleo
yetu”
 
Bw
Nkwera alisema kwa kazi  iliyofanywa na mbunge  huyo katika  jimbo la
Ludewa  kwa  kipindi cha  miaka 5 ni  kubwa zaidi na inaweza imezidi
hata ile ya  wabunge waliokaa madarakani zaidi ya miaka 40 bila kufanya 
kazi kubwa kama  hiyo ya mbunge wa Ludewa.
 
Hata  
hivyo  alisema ili Ludewa  izidi kusonga mbele  zaidi hakuna  sababu ya
wana Ludewa kufanya  siasa za maeneo mengine za kuvutana kwenye mambo
ya maendeleo kwani  kufanya   hivyo  ni kujikwamisha zaidi katika
maendeleo kama  ilivyo kwenye majimbo mengine ambayo wabunge  wanafanya
kazi katika mazingira magumu na wafuasi  wa chama cha  upinzani
hawatakiwi katika shughuli za CCM na wale wa CCM hivyo hivyo  japo kwa
Ludewa kwenye mambo ya  kimaendeleo  ni wananchi  wote  na  vyama 
vinawekwa kando.
 
Mwenyekiti
wa  serikali  ya  kijiji  cha Luana Bw David  Luoga alisema kuwa
wananchi  hao kamwe hawatamsahau  mbunge  huyo kwani ameweza
kuwaharakishia maendeleo ya  kijiji hicho  kwa  kufikisha umeme na
kuwatengenezea barabara   hiyo ya  Malatu – Itungi  ambayo ilikuwa
haipitiki japo  inaelekea katika taasisi mbali mbali kama nyumba  za
ibada, soko, Zahanati  na shule  ila serikali ya wilaya haikuona sababu
ya  kuitengeneza hadi wananchi  hao  walivyoomba  kwa  mbunge  huyo
katika mkutano wao wa hadhara  uliofanyika miezi mitatu  iliyopita .
 
Bw
Luoga  alisema  toka  nchi  ipate  uhuru wake  mwaka 1961 kijiji  hicho
hawajapata barabara nzuri kama  hiyo ambayo ni barabara muhimu ambayo
haikupewa umuhimu  wowote na  serikali ya wilaya ya  Ludewa.
 
Hivyo
alisea ahsante  yao kwa  mbunge wao kwa  kuwaletea maendeleo ni  kuona
wanamchagua kwa  kura  nyingi zaidi  ili kuendelea kuwa mbunge kwa
vipindi vingine 15 ama  zaidi   na  kuwa kipimo chake   kilikuwa ni
miaka  mitano  hii ambayo ameonyeha ufaulu  wa  zaidi ya asilimia 100
hivyo kama kijiji wananchi wameweza  kuchangishana  na  kupata kiasi cha
Tsh 100,000 kwa  ajili ya kwenda  kuchukulia fomu muda  wa  kufanya
hivyo utakapofika.
 
Kwa
upande  wake  mbunge Filkunjombe pamoja na  kuwapongeza  wananchi hao
wakiwemo wale  wa Chadema ambao  walijitolea  kushirikiana  nae katika
ujenzi  wa barabara   hiyo bado alimpongeza mkurugenzi  wa kampuni ya
barabara  ya Boimanda chini ya mkurugenzi  wake Nicholaus Mgaya kwa 
kuendelea   kuwa mzalendo na wilaya ya Ludewa kwa kujitolea  mitambo ya
kuchonga barabara hiyo  bila malipo.
 
Alisema
ni wakandarasi  wachache  sana  wazalendo ambao wanajitolea kwa
wananchi kama   hivyo na  kuwa kampuni  hiyo si  tu imekuwa ikijitolea
katika jamii bali ni  moja kati ya kampuni za kizalendo ambazo zinafanya
kazi ya  ujenzi wa barabara kwa uaminifu mkubwa bila  kulipua kama
zilizokampuni nyingine za ukandarasi ambazo hugeuza wilaya   hiyo  ya
Ludewa ni shamba la bibi kwa kujenga barabara kwa kiwango  cha chini ili
mradi  wachume pesa.
 
Mbunge
Filikunjombe aliwataka  wananchi hao  wa Luana kutunza barabara   hiyo
badala ya kuiharibu kwa kupitisha mifugo na  kuwa kutengenezwa kwa
barabara  hiyo  kutapunguza maswali ya  wananchi katika mikutano ya
hadhara kwa  wananchi hao kila mkutano kutoa  kilio cha barabara  hiyo
huku akisisitisha  kuwa  kero  zipo  nyingi haziwezi  kumalizika zote
kwa  wakati mmoja japo kwa kuchagua moja  moja ipo siku zitamalizika 
zote .
 
“Leo  kikao  cha  bunge kinaendelea bungeni ila nimeona  ni vizuri kukimbia mara moja kuja  kutatua kero  hiyo ya barabara ambayo ilikuwa ikiwatesa  wananchi  wangu kwanza …..kwani  ubunge huu  ni wa  wananchi hivyo  lazima  pale ninapoweza kuwasaidia kero  zao”
 
Wakati  
huo  huo  mbunge Filikunjombe amewapongeza wananchi  wa Luana  kwa
kumchangia kiasi hicho cha pesa za  kuchukulia fomu pia kumpongeza
mwenyekiti  wa  BAVICHA  kwa kujitoa kwake katika  shughuli  za
maendeleo pasipo kutanguliza itikadi  za chama chake na  kuwataka  wana
Ludewa kushikamana katika mambo ya kimaendeleo badala ya  kujikita
katika siasa za kupinga maendeleo kama ilivyobaadhi ya majimbo hapa
nchini.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles