Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

BURUNDI: WAANDAMANAJI WAKATA TAMAA BAADA YA MKUTANO WA DAR ES SALAAM

$
0
0
Mtoto huyo anaangalia jinsi askari polisi wakiondoa vizuizi viliyowekwa kwenye barabara za mji wa Bujumbura, Mei 30 mwaka 2015.
Mtoto huyo anaangalia jinsi askari polisi wakiondoa vizuizi viliyowekwa kwenye barabara za mji wa Bujumbura, Mei 30 mwaka 2015.
Na RFI
Baada ya mkutano wa marais wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki uliyofanyika Jumapili Mei 31 jijini Dar es Salaam, nchini Tanzania, raia katika wilaya za mji wa Bujumbura, nchini Burundi, hasa waandamanaji wamekata tamaa kufauatia uamzi wa marais hao.
Suala muhimu la awamu ya tatu ya Rais Pierre Nkurunziza halikuchukuliwa uamzi katika mkutano huo au
hata kujadiliwa na marais hao wa nchi za Afrika Mashariki. Watu wamechukizwa na jambo hilo na wako tayari kuendelea na maandamano.
Katika wilaya za mji wa Bujumbura kunakofanyika maandamano kama Cibitoke na Nyakabiga, raia wamekata tamaa. Lakini pia wamekua na hasira, baada ya mapendekezo yaliyotolewa katika mkutano wa jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki.(P.T)

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles