Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

HOFU YA EBOLA YATANDA MKOA WA IRINGA

$
0
0

Mwili  wa mgonjwa wa Ebola  ukitolewa Wodini huku Liberia picha na maktaba

WAKATI ukimwa  wa ugonjwa  wa  Ebola  ukiwa  umetawala  wakazi  wa mji  wa  Iringa  mkoani  Iringa    wapo  katika  hofu  kubwa kufuatia  kuwepo kwa taarifa ya  mgonjwa  wa  Ebola  kufariki katika  Hospitali ya  Rufaa ya  mkoa  wa  Iringa.
Taarifa  ambazo bado  kuthibitishwa na wizara ya  afya  zinadai  kuwa  mgonjwa   huyo alikuwa amwelazwa wodi namba  8  katika Hospitali  hiyo ya  Rufaa ya  mkoa wa Iringa na baada ya  kifo  chake  chenye  shaka ya  ebola  vipimo  vimechukuliwa na kupelwekwa kwa mkemia  mkuu wa serikali  ili kuweza  kutoa  majibu  sahihi .
Mbali ya  vipimo  hivyo  kuchukuliwa  tayari  ndugu wa  mgonjwa  huyo  wanadaiwa  kuteketeza  nguo  zake kwa  moto kwa  hofu ya  kuambukizwa  ugonjwa  huo  hatari na hadi sasa mwili  wa marehemu huyo  upo  katika chumba  cha  kuhifadhia maiti katika  Hospitali  hiyo  ya Rufaa ya  mkoa  wa Iringa.
Mtandao   wa www.matukiodaima.co.tz  usiku  wa Jana  umetinga katika  hospitali  hiyo  ya Rufaa ya  mkoa  wa  Iringa na kupata taarifa za awali  kutoka  wodi 8 kuwa ni kweli  kuna  mgonjwa ametiliwa  shaka na  uchunguzi unaendelea na hadi kesho majibu  yatapatikana .
 
Kwa hisani ya francisgodwin.blogspot



Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles