Na Gabriel Kilamlya Njombe
Mkuu Wa Mkoa wa Njombe Dokta Rehema Nchimbi Amewataka Wakulima Kwenda Kuketi Katika Meza ya Mazungumzo na Wafugaji Ili Kumaliza Tofauti Zao za Migogoro ya Ardhi.
Kauli Hiyo Ameitoa Februari 20 Mwaka Huu Katika Mkutano Mkuu wa Mtandao wa Vikundi Vya Wakulima MVIWATA Mkoa wa Njombe na Iringa Uliofanyika Katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Mjini Njombe Kwa Kushirikiana na Mikoa ya Iringa,Mbeya na Ruvuma Ambao Pia Umefanya Uchaguzi wa Kuwachagua Viongozi Wapya wa MVIWATA.
Dokta Nchimbi Amesema Ufike Wakati Sasa Wakulima Wakubali Kufanya Mazungumzo na Wafugaji na Kuwataka Kumaliza Tofauti Zao na Kwamba Miongoni Mwa Sababu Zinazochangia Wafugaji Kuendeleza Malumbano Hayo ni Kutokana na Wao Kushindwa Kuvuna Mifugo Yao Kama Wakulima.
Pamoja na Mambo Mengine Dokta Nchimbi Amewaonya Wanasiasa Kuacha Tabia ya Kuwadanganya Wakulima na Wanachi Kwa Ujumla Hususani Katika Kipindi Hiki Cha Kuelekea Katika Zoezi la Uandikishaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Akisoma Risala ya MVIWATA Mratibu wa Mtandao Huo Kwa Mkoa wa NJombe na Iringa Bwana Venacy Ngimbudzi Amesema Kuwa MVIWATA Imekuwa Mkombozi Kwa Wakulima Wengi Nchini Tanzania Tangu Kuanza Kwake Mwaka 1993 Ikiwa Hadi Sasa Unajumla ya Wanachama 7546.
Habibu Simbamkuti ni Mwenyekiti Mstaafu wa MVIWATA Taifa na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Mviwata Ambaye Amewataka Wakulima Hao Kufanya Uchaguzi Kwa Kuwachagua Viongozi Bora Watakaosaidia Kutatua Migogoro Baina ya Wakulima Hao na Wafugaji.