Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

WAKAZI NJOMBE WASHANGAZWA KUTOSHUKA KWA BEI YA NAULI WAKATI MAFUTA YAMESHUKA

$
0
0

 

















Na Gabriel Kilamlya NJOMBE

Wakati Serikali Ikishusha Bei ya Mafuta Kwenye Vituo Mbalimbali Hapa Nchini,Wananchi Mkoani Njombe Wameshangazwa Kuona Hadi Sasa Nauli za Mabasi Hazijashuka.

Wakizungumza Kwa Nyakati Tofauti na www.gabrielkilamlya.blogspot.com Baadhi ya Wananchi na Abiria wa Mabasi Hayo Wamesema Kuwa Wanashindwa Kufahamu Dhana ya Serikali Kushusha Bei ya Mafuta  Kwani Inawapa Wakati Mgumu Kutokana na Gharama Kubwa za Nauli Pindi Wanaposafiri.

Katika Hatua Nyingine Mwandishi wa Mtandao Huu Umefanya Mazungumzo na Baadhi ya Maafisa Usafirishaji Katika Kituo Kikuu Cha Mabasi Mjini Njombe Ambao Wamesema Kuwa Kutokana na Ubovu wa Miundombinu ya Barabara Hususani za Vumbi Pamoja na Gharama za Uendeshaji Wanashindwa Kushusha Bei Hizo.

Pia Wamesema Wanashindwa Kushusha Bei Hizo Kwa Kuwa Wao Sio Wamiliki wa Mabasi Hayo na Kwamba Wanafuata Muongozo wa Mmiliki wa Chombo Husika.

Kutokana na Hali Hiyo mtandao huu Umelazimika Kumtafuta Afisa Mfawidhi wa Sumatra Mkoa wa Njombe Bwana Joseph Burongo Ambaye Amesema Kuwa Kwa Sasa Hawawezi Kushusha Nauli ya Mabasi Hayo  Kutokana na Mafuta Hayo Kushuka Kwa

Asilimia Kumi Pekee Ambayo Inaendelea Kuwapa Ugumu Wamiliki wa Magari  Hayo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles