MWANASHERIA MSAIDIZI WA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE BAHATI KIKOTI
HAPA NI MTAA WA MGENDELA ZOEZI LA KUAPISHWA LILIFANYIKA LEO
Akizungumza Na Wenyeviti, Wajumbe Pamoja Na Baadhi Ya Wananchi Wakati Wa Kuanza Zoezi Hilo La Kuapisha Viongozi Wa Serikali Za Mitaa Kata Ya Njombe Mjini Hakimu Wa Mahakama Ya Mwanzo Izack Mlowe Amepongeza Kwa Kuchaguliwa Kwa Viongozi Hao Na Kwamba Mara Baada Ya Kuapishwa Viongozi Hao Wanatakiwa Kufuata Maadili Ya Uongozi .
Hakimu Huyo Wa Mahakama Ya Mwanzo Mlowe Amesema Kuwa Viapo Walivyopewa Ni Vya Kuanza Utekelezaji Rasmi Wa Majukumu Ya Serikali Za Mitaa Na Vijiji Kwa Kufuata Katiba Ya Nchi,Sheria Za Nchi ,Taratibu Za Nchi Na Maadili Ya Umma Ambapo Amesema Hategemei Kiongozi Yeyote Ambaye Atakiuka Kiapo Walichopewa.
Awali Akimkaribisha Hakimu Wa Mahakama Ya Mwanzo Mjini Njombe Izack Mlwe, Mwanasheria Msaidizi Wa Serikali Wa Halmashauri Ya Mji Wa Njombe Bahati Kikoti Amesema Kuwa Lengo La Kuwaapisha Ni Kutokana Na Kuwepo Kwa Matakwa Ya Sheria Inayowataka Kutekeleza Zoezi La Kuapisha Viongozi Waliochaguliwa Ili Kuanza Kutekeleza Majukumu Yao.
Afisa Mtendaji Wa Kata Ya Njombe Mjini Bonasius Mwalongo Amesema Kuwa Baada Ya Halmashauri Ya Mji Wa Njombe Kufanya Zoezi La Kuwaapisha Viongozi Hao Wa Mitaa Halmashauri Hiyo Inatarajia Kwenda Kwa Awamu Nyingine Kuwapatia Semina Viongozi Hao Kwa Kuwa Halmashauri Kwa Sasa Haina Bajeti Ya Fedha Ya Kutolea Semina Hiyo Ambapo WanatakiwaKutekeleza Majukumu Yao Kusimamia Amani Na Utulivu.
Kwa Upande Wao Baadhi Ya Wajumbe Na Wenyeviti Walioapishwa Wamezungumzia Mipango Mikakati Ambayo Itawekwa Kuwa Ni Pamoja Na Kuanza Zoezi La Kuimarisha Ulinzi Shirikishi Pamoja Na Kutekeleza Miradi Ya Mitaa Kwa Kupata Maoni Kutoka Kwa Wananchi Kwa Kushirikiana Na Viongozi Wa Mitaa Jirani Pamoja Na Wananchi Wao.
HUYU NI MWENYEKITI WA MTAA WA KAMABALAGE