"Namshukuru Mwenyezi Mungu, Lakini Pia Nawashukuruni Nyote Kwa Sala Zenu Na Dua Zenu Zilizoniwezesha Hata Kusimama Hapa Mbele Yenu Saa Hizi Kama Mnavyoniona," Alisema Huku Akishangiliwa Na Mamia Ya Waumini Wa Kanisa Hilo.
Askofu Mkuu Wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu La Dar Es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo Amesema Kuwa Hali Ya Afya Yake Inaendelea Kuimarika. Na Kuwataka Waumini Kuendelea Kumwombea.
Akizungumza Kwenye Misa Takatifu Ya Mavuno Na Shukurani Kwa Jimbo Hilo, Iliyofanyika Jana Msimbazi Center Jijini Dar Es Salaam, Pengo Alisema Ameamua Kuitumia Siku Hiyo Kumshukuru Mungu Kwa Kuwa Ndiye Alimfanya Kuwa Hai Hadi Sasa.
"Namshukuru Mwenyezi Mungu, Lakini Pia Nawashukuruni Nyote Kwa Sala Zenu Na Dua Zenu Zilizoniwezesha Hata
Kusimama Hapa Mbele Yenu Saa Hizi Kama Mnavyoniona," Alisema Huku Akishangiliwa Na Mamia Ya Waumini Wa Kanisa Hilo.Alitumia Muda Huo Kuwaasa Waumini Kuwa Na Tabia Ya Kushukuru Kutoka Ndani Ya Mioyo Yao, Akisema Ndilo Jambo Linalompendeza Mungu.(P.T)
kwa hisani ya mjengwablog