Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Article 4

$
0
0

MBUNGE PETER MSIGWA ATOA MSADA CHUO CHA KIISLAMU IRINGA.

Mchungaji Msigwa akikabidhi msaada kwa Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Iringa, Abubakari Chalamila 
ZIKIWA zimebaki siku chache kwa waislamu nchini kuungana na waislamu dunia kote kusheherekea siku kuu ya Idd El Fitri, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) ametoa msaada kwa Chuo cha Kitanzani Islamic Center.

Msaada huo unahusisha Kilo 750 za Sukari, Kilo 250 za Unga wa Ngano, katoni 50 za Tende na Katoni 50 za mafuta ya kupikia ikiwa ni utaratibu wake wa kila mwaka kukisaidia chuo hicho.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo jana kwa Sheikh Mkuu wa Mkoa Iringa Abubakar Chalamila, Mchungaji Msigwa alisema ametoa msaada huo kwa lengo la kuwaunga mkono waislamu katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani na kuwakumbuka wanaoishi katika mazingira magumu.

Mchungaji Msigwa alisema wadau wana jukumu ka kuwasaidia wale wote wanaohitaji bila kujali itikadi za vyama.
  
Akishukuru kwa niaba ya chuo hicho, Sheikh, Abubakar Chalamila alisema; “namshukuru sana Msigwa kwa msaada huu na tunamuahidi utafikishwa kwa walengwa.” Alisema.

Chalamila aliwataka wadau wengine kuwakumbuka watu wasiojiweza na wanaoishi katika mazingira magumu mara kwa mara kwani kwa kufanya hivyo wanajiongezea thawabu.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles