Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all 2276 articles
Browse latest View live

Article 16


Article 15

$
0
0

KITUO CHA NURU OPHANS CHAKABIDHI VITENDEA KAZI KWA VIJANA WANAOISHI KWENYE MAZINGIRA MAGUMU MBEYA

 Venance Matinya kutoka  mtandao wa Mbeya yetu Blog  akipokea Hati ya shukrani kutoka kwa Mgeni Rasmi Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Mbeya, Thobias Mwalwego kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa kwa kutambua mchango wa Mbeya yetu  Blog katika kulea watoto yatima

 mwanafunzi aliyehitimu fani ya ufundi wa magari akikabidhiwa vifaa vyake.
 Mwanafunzi aliyehitimu fani ya kilimo cha mbaogamboga akikabidhiwa vitendea kazi.
 Mwanafunzi wa fani ya useremala naye akikabidhiwa vitendea kazi.
 Mgeni rasmi, Afisa ustawi wa jamii Mkoa wa Mbeya, Thobias Mwalwego akihutubia katika hafla hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro.

Mwanafunzi wa fani ya ushonaji akikabidhiwa vitendea kazi ambacho ni Cherehani.
  Meneja wa Kituo, Amanda Fihavango akiwaeleza jambo waandishi wa habari
.Mkurugenzi wa Nuru Orphans centre Jasson Fihavango akisoma risala.
 Mwanafunzi akikabidhiwa cheti cha kuhitimu masomo yake.
Wageni waalikwa wakitembelea majengo ya kituo cha nuru.

KITUO cha Nuru Ophans kimekabidhi vitendea kazi kwa vijana wanaoishi kwenye mazingira magumu Mbeya baada ya kuhitimu mafunzo ya fani mbali mbali kutoka Chuo cha ufundi Veta mkoani Mbeya.
 
Hafla hiyo ilifanyika juzi katika makao makuu ya kituo hicho kilichopo Uyole Jijini Mbeya ambapo vijana 30 walipewa vyeti vya kuhitimu masomo yao pamoja na vifaa vya kufanyia kazi.
 
Meneja Miradi wa Nuru Ophans Centre, Osward Poyo,alisema Asasi yake baada ya kufanya utafiti ilibaini kuwepo kwa vijana wanaoishi katika mazingira magumu  2500 katika kata 6.
 
Alisema baada ya kubaini hayo Asasi hiyo iliomba msaada kwa Ubalozi wa Marekani nchini kwa ajili ya kuwasomesha vijana hao fani mbali mbali za ufundi lakini Ubalozi ulikubali kuwasomesha vijana 30 tu hivyo kufanya kila kata kutoa vijana 5.
 
Aliongeza kuwa Ubalozi wa Marekani baada ya kutiliana sahihi mkataba wa kuwasomesha vijana hao walitoa jumla ya shilingi 16,800,000 kwa malipo ya ada, Nauli ya kwenda na kurudi chuoni, malipo ya chakula kwa siku zote za masomo na ununuzi wa Vitendea kazi kulingana na fani ambazo vijana wamesomea.
 
Alizitaja fani ambazo vijana hao wamesomea na vifaa walivyokabidhiwa kuwa ni pamoja na fani ya Ushonaji ambayo ilikuwa na vijana 12 waliokabidhiwa Cherehani kila mmoja,Seremala kijana mmoja aliyekabidhiwa Misumeno 3,Landa 2, Nyundo pamoja na Ovaroli.
 
Wengine ni fani za Ufundi magari ambao ulikuwa na vijana 6 ambao kila mmoja alikabidhiwa Ovaroli,dazani ya spana na Jeki ya kuinulia magari na vijana 9 waliochukua fani ya udereva ambao walipewa Leseni za kuendeshea magari na vijana wawili waliosoma fani ya klilimo cha mboga mboga ambao walipewa kila mmoja kilo 50 za mbolea aina ya Urea, Mbegu za mahindi kilo 6, Pumpu ya kunyunyizia dawa 1 pamoja na mbegu za mboga za nyanya, spinachi na karoti.
 
Naye Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Afisa ustawi wa jamii Mkoa wa Mbeya,Thobias Mwalwego, ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, alitoa wito kwa vijana wa fani za ufundi kuwa waaminifu kwa wateja wao na huduma watakazokuwa wakitoa kwa manufaa ya jamii nzima.
 
Alisema vifaa walivyokabidhiwa vinafaa kutunzwa na siyo kukimbilia kuuza hali ambayo inaweza kuwarudisha katika hali ya awali ya kuzurura mitaani bila kuwa na fani ya kufanya.

Na mwandishiwetu

Article 14

$
0
0

TUNDU LISU AWATAJA MAWAZIRI,WABUNGE WALIOOMBA FEDHA


Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amewataja kwa majina mawaziri na wabunge aliosema bungeni kuwa wamekuwa ombaomba katika mifuko ya hifadhi ya jamii.
 
Baadhi ya waliotajwa ni pamoja na Mbunge wa Kongwa ambaye pia ni Naibu Spika, Job Ndugai; Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu wa Bunge), William Lukuvi; Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Pindi Chana na wabunge Betty Machangu (Viti Maalumu), Livingstone Lusinde (Mtera), John Komba (Mbinga Magharibi), Eugen Mwaiposa (Ukonga) na Gudluck Ole Medeye (Arumeru Magharibi).
 
Hata hivyo, gazeti hilo halijawataja majina mawaziri na wabunge wengine waliomo kwenye orodha hiyo ya Lissu kwa kuwa hawakupatikana jana kujibu tuhuma hizo.
Mbali na kuwataja kwa majina, Lissu pia ametoa vielelezo vinavyoonyesha jinsi walivyokuwa wakiidhinishiwa malipo kwa nyakati tofauti na Mfuko wa Pensheni kwa Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (LAPF), kwa sababu mbalimbali.
Lissu alimwambia mwandishi wetu jana kuwa licha ya kiwango cha fedha kutokuwa kikubwa, lakini kinaweza kusababisha mgongano wa kimasilahi kati ya wajibu wa wabunge kwa umma na masilahi yao binafsi.
"Hali hii inaweza kusababisha Bunge likashindwa kutimiza wajibu wake wa kikatiba wa kuisimamia Serikali na taasisi zake," alisema Lissu huku akisisitiza azimio lake la kuwasilisha hoja binafsi kwa Spika wa Bunge ili iundwe tume kuchunguza suala hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa LAPF, Eliud Sanga jana alikiri kuwa shirika hilo liliidhinisha malipo kwa mawaziri na wabunge hao kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo.
Hata hivyo, alisema shirika hilo halitoi fedha taslimu, bali hununua vitu ambavyo viliombwa na viongozi hao kwa ajili ya kusaidia wananchi na si kufanya biashara.
Sakata lenyewe
Akizungumzia jinsi mawaziri na wabunge hao walivyosaidiwa, Lissu alisema LAPF ilitoa Sh2.5 milioni kwa ajili ya mradi wa madarasa Jimbo la Kongwa linaloongozwa na Ndugai.
Alipoulizwa kuhusu madai hayo, Ndugai alisema hakuna tatizo lolote kwa mbunge kupewa msaada na mfuko wa kijamii.
"Huyo Lissu ana upungufu mkubwa. Hivi LAPF ikisaidia Sh2 milioni kwa ujenzi wa darasa unaogharimu Sh10 milioni ni tatizo hilo? Nchi hii inakwenda wapi jamani, siyo kila kitu wanachozungumza wapinzani ni hoja, kama LAPF wangekuwa wanatoa fedha lingekuwa tatizo lakini wanasaidia vifaa tu."
CHANZO:MWANANCHI

MTOTO WA MKULIMA

$
0
0
PG4A0268Waziri mkuu mizengo Pinda akifurahia mavuno yake.

Article 12

$
0
0
WABUNGE WAMUWASHIA MOTO MWAKYEMBE-WIZARA YA UCHUKUZI.
 Waziri wa Uchukuzi Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe na Mhe Anna Abdallah wakiwa   na Marubani  wanawake waliotembelea Bunge  kufuatilia  Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi kwa Mwaka 2014/2015 leo.
 Waziri wa Uchukuzi Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe akijibu hoja za Wabunge kuhusu Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi kwa Mwaka 2014/2015 leo.
 Waziri wa Uchukuzi Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe na Mhe Anna Abdallah wakiwa na madereva wa Treni wanawake waliotembelea Bunge  kufuatilia  Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi kwa Mwaka 2014/2015

 Waziri wa Uchukuzi Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe na Mhe.Pindi Chana Naibu waziri wa Maendeleo ya Jamii wakiwa katika  picha ya pamoja na  Marubani  (wanawake),Kapteni wa Meli,madereva wa Treni (wanawake) na Marubani (wanawake) .waliotembelea Bunge leo kufuatilia  Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi kwa Mwaka 2014/2015 leo.

 Waziri wa Uchukuzi Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza na baadhi ya watumishi wa wizara yake waliotembelea Bunge  kufuatilia  Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi kwa
Mwaka 2014/2015. 

Na Deusdedit Moshi Mtendaji Mkuu wa Photo Solutions wawakilishi wa Michuzi Blog Kanda ya kati. 

Article 11

$
0
0

JINSI MWENYEKITI WA CCM WILAYA YA NJOMBE ALIVYOZIKWA KIJIJINI LUSITU HUKO LUPONDE

 Deo Sanga ambaye ni Mbunge na Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Njombe akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Njombe.



 Aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Njombe,Adam Ismail Msigwa (pichani) ambaye alijukana kwa jina maarufu kama 'Shilingi ni Vita' amefariki  nyumbani katika Mitaa wa Kwivaha Njombe mjini na mazishi yalifanyika katika kijiji cha lisitu.

Mkuu wa mkoa wa Njombe Cept. mstaafu Aseri Msangi (kushoto ) wa pili ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Bw Saitabau na wa mwisho (kulia) ni Kamanda wa polisi mkoa  SACP  Ngonyani.

"MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU PEMA PEPONI"

 'AMINA'
PICHA ZOTE NA  PROSPER MFUGALE.

Article 10

$
0
0

WANANCHI WA KIJIJI CHA IKHOHO MBEYA WAWATUHUMU VIONGOZI WAO KWA KUTUMIA VIBAYA FEDHA ZA MICHANGO.


Baadhi ya wanakijiji na Wanausalama wakifuatilia kwa Makini Kikao hicho.

*******
UONGOZI wa  Kijiji cha Ikhoho Kata ya Maendeleo Wilaya ya Mbeya unatuhumiwa kufuja fedha za michango ya maendeleo zaidi ya shilingi milioni tatu zilizochangwa na wananchi pamoja na matumizi mabaya ya madaraka.
 
 
Tuhuma hizo zilitolewa jana mbele ya mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo ambao ulihudhuriwa na Polisi Tarafa,Mkaguzi wa Polisi Galusi Ligula, pamoja na  Mwenyekiti wa Kijiji aliyeondolewa madarakani, January Mwambole na Mtendaji wa Kijiji, Wakaa Nkembo.
 
 
Wakizungumza kwenye mkutano huo wananchi wamedai kuwa kwa kutumia madaraka yao viongozi hao waliwatoza wanafunzi 45 wa shule ya msingi ya kijiji hicho shilingi 525,000/- wanafunzi wakidaiwa kuvunja choo cha shule.
 
 
Walisema Wanafunzi 40 walitozwa shilingi elfu tano kila mmoja katika ofisi ya kijiji na wanafunzi watano wakilipa shilingi elfu sitini na tano katika Kituo cha Polisi cha Inyala ambapo waliwekwa mahabusu kabla ya wazazi wao kulipa pesa hizo.
 
 
Waliongeza kuwa kwa kutumia madaraka yao viongozi hao walianza kuwaandama wananchi waliokuwa wakihoji uhalali wa tozo hilo ambapo kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Bahati Kitundu alifunguliwa jalada la kutishia kufanya fujo kijijini kutokana na kuandika barua ya malalamiko kwa Mkuu wa Wilaya ya Mbeya juu ya kero za michango mbalimbali Kijijini hapo.
 
 
Wananchi hao walisema mbali ya pesa za choo cha shule ya Msingi viongozi hao wanatuhumiwa kutafuna michango ya ujenzi wa shule ya Sekondari ya Ikhoho ambazo walikusanya kutoka kwa wananchi na kutoziwasilisha sehemu husika kwa muda mrefu na baadhi ya wananchi walikamatwa kwa kushindwa kutoa pesa hizo kwa wakati.
 
Aidha katika mkutano huo Jeshi la Polisi lilitumia fursa ya kutoa elimu kwa wananchi kutotumia mabavu katika shughuli za maendeleo na viongozi watimize majukumu yao.

Baada ya kumalizika kwa mkutano huo wananchi hao waliazimia kuunda tume ya watu watano kwa ajili ya kujiridhisha na tuhuma hizo kabla ya kuwasimamisha kazi viongozi wa Kijiji
 
Na Mbeya Yetu

Article 9

$
0
0

WASHINDI "TANAPA MEDIA AWARDS 2013 "WAPATIKANA WAKABIDHI ZAWADI

Mshereheshaji Sauda Simba Kilumanga akiwakaribisha wageni katika ukumbi wa JB Belmont jijini Mwanza kwa ajili ya sherehe za utolewaji wa Tuzo kwa Wanahabari zinazoandaliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa,Tanzania(TANAPA)Paschal Shelutete akifanya utamburisho wa wageni mbalimbali waliofika katika shughuli hiyo.
Baadhi ya wageni mbalimbali katika shughuli hiyo.
Meza kuu iliongozwa na Waziri wa Maliasili na Mazingira ,Lazaro Nyarandu.
Waziri Nyarandu akiteta jambo na Mkurugenzi wa Utalii na Masoko wa TANAPA,Ibrahim Mussa.
Mmoja kati ya wageni waalikwa alikuwa ni Mkurugenzi wa Umoja wa vilabu vya Waandishi wa Habari nchini ,Abubakar Karsan ambaye alipata nafasi ya kuzungumza machache.
Kiongozi wa Majaji waliofanya kazi ya kupitia kazi za Waaandishi walioshindanishwa na kisha kupatikana washindi Dk Ayoub Rioba akizungumza namna washindi walivyopatikana na baadae kuwatambulisha Majaji wenzake.
Majaji walioshiriki kufanya kazi ya kupitia kazi za washiriki .
Wageni mbalimbali wakifutilia shughuli hiyo.
Mgeni rasmi katika sherehe za utolewaji wa Tuzo zijulikanazo kama TANAPA Media Award 2013,Waziri wa Maliasili na Utalii ,Lazaro Nyarandu ,akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa,Allan Kijazi,Mkurugenzi wa Utalii na Masoko Ibrahimu Mussa pamoja na Meneja Ujirani Mwema Ahmed Mbugi tayari kwa zoezi la utolewaji wa TUZO HIZO.
Mgeni rasmi katika sherehe za utolewaji wa Tuzo zijulikanazo kama TANAPA Media Award 2013,Waziri wa Maliasili na Utalii ,Lazaro Nyarandu akitoa mfano wa Hundi ya kiasi cha Sh Milioni moja na laki tano kwa mshindi namba mbili wa uandaaji wa vipindi vya Radio,Humphrey Mgonja wa Radio SAUT fm.

Mgeni rasmi katika sherehe za utolewaji wa Tuzo zijulikanazo kama TANAPA Media Award 2013,Waziri wa Maliasili na Utalii ,Lazaro Nyarandu akikabidhi mfano wa Hundi ya kiasi cha Sh Milioni mbili pamoja na Ngao kwa mshindi namba moja wa uandaaji wa vipindi vya Radio,David Rwenyagira wa Radio 5 FM.

Mgeni rasmi katika sherehe za utolewaji wa Tuzo zijulikanazo kama TANAPA Media Award 2013,Waziri wa Maliasili na Utalii ,Lazaro Nyarandu akitoa mfano wa Hundi ya kiasi cha Sh Milioni moja kwa mshindi namba tatu kwa waandaji wa vipindi vya Televisheni ,Kakuru Msimu wa Star TV.

Mgeni rasmi katika sherehe za utolewaji wa Tuzo zijulikanazo kama TANAPA Media Award 2013,Waziri wa Maliasili na Utalii ,Lazaro Nyarandu akitoa mfano wa Hundi ya kiasi cha Sh Milioni moja kwa mshindi namba tatu upande wa Magazeti ,Salome Kitomary wa gazeti la Nipashe.

Mgeni rasmi katika sherehe za utolewaji wa Tuzo zijulikanazo kama TANAPA Media Award 2013,Waziri wa Maliasili na Utalii ,Lazaro Nyarandu akitoa mfano wa Hundi ya kiasi cha Sh Milioni moja na laki tano kwa mshindi namba mbili kwa waandaji wa vipindi vya Televisheni ,Raymond Nyamwihula wa Star TV.
Mgeni rasmi katika sherehe za utolewaji wa Tuzo zijulikanazo kama TANAPA Media Award 2013,Waziri wa Maliasili na Utalii ,Lazaro Nyarandu akitoa mfano wa Hundi ya kiasi cha Sh Milioni mbili pamoja na Ngao kwa mshindi namba moja  kwa waandaji wa vipindi vya Televisheni ,Vedasto Msungu wa ITV.
Baadae David Rwenyagira alipata nafasi ya kutoa neno la shukrani kwa niaba ya washidi wa tuzo hizo.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la hifadhi za Taifa ,Tanzania ,Allan Kijazi akitoa neno na kisha kumkaribisha mgeni rasmi katika shughuli hiyo ,Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyarandu.
Mgeni rasmi katika sherehe za utolewaji wa Tuzo zijulikanazo kama TANAPA Media Award 2013,Waziri wa Maliasili na Utalii ,Lazaro Nyarandu akitoahotuba yake mara baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa tuzo.
Mwanamuziki Nguli wa muziki wa Bendi hapa nchini King kii a.k.a Mzee wa Kitambaa Cheupe na bendi yake alitoa burudani kwa washindi pamoja na wageni waalikwa.
Kila mmoja aliweka kitambaa Cheupe juu.
Baadae likafuatia neno la shukrani toka kwa Mkurugenzi wa Utalii na Masoko ,Ibrahimu Mussa.

BREAKING NEWZZZZZZZZZZZZ

$
0
0
DIWANI WA KATA YA MFIRIGA[CCM],H/WILAYA YA NJOMBE Ndg.KAMILO HONGOLI AFARIKI DUNIA alfajiri ya Leo.
Diwani wa kata ya Mfiriga[CCM] Kamilo Hongoli Enzi za Uhai Wake

Na Gabriel  Kilamlya Njombe

Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mfiriga Wilayani Njombe Kamilo  Hongoli Amefariki Dunia Usiku wa Kuamkia Leo Akiwa Anapatiwa Matibabu Katika Hospitali ya Ikonda Wilayani Makete.

Akizungumza Juu ya Kifo Cha Diwani Huyo Leo,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Bwana Valence Kabelege Amesema Kuwa Diwani Hongoli Amefariki Akiwa Anapatiwa Matibabu ya Maradhi ya Ugonjwa wa Malari Katika Hospitali ya Ikonda.

Aidha Bwana Kabelege Amesema Kuwa Awali Diwani Huyo Alilazwa Katika Hospitali Hiyo ya Ikonda na Kisha Kurejea Katika Hali Yake Lakini Homa Ikamrudia Tena Hadi Mauti Yanamkuta Alikuwa Anasumbuliwa na Maumivu Ya Mwili Mzima Pamoja na Malaria.

Amesema Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Imempoteza Kiongozi Muhimu Katika Maendeleo ya Jamii na Taifa Kwa Ujumla Kwani Alikuwa Kiungo Muhimu Kati ya Wananchi na Serikali Ndani ya Kata Ya Mfiriga.

Katika Hatua Nyingine Bwana Kabelege Amesema Kuwa Mara Baada ya Kuagwa Mwili Wake Katika Eneo Alilokuwa Akiishi Jirani na Shule ya Sekondari Joseph Mbeyela Mwili Wake Utasafirishwa Hadi Kijijini Kwake Mfiriga Kwa ajili ya Mazishi Yatakayofanyika Hapo Kesho.

Marehemu Camilo Hongoli Amekuwa Diwani Katika Kata Hiyo Ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Tangu Mwaka 2005 Hadi Mauti Yanamkuta Alikuwa Akiongoza Kata Hiyo Ya Mfiriga.

Mtandao huu Unatoa Pole Kwa Ndugu Jamaa na Marafiki Pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Kwa Kuondokewa na Kiungo Muhimu Katika Taifa.

Mungu Ailaze Roho Ya Marehemu Kamilo Hongoli Mahali pema Peponi   Ameeeen!
............................................................................................................

Article 7

$
0
0

WATU WATATU WAFARIKI KTK MATUKIO TOFAUTI MKOANI IRINGA.

Watu watatu wafariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa katika matukio tofauti tofauti mkoani Iringa likiwemo la abiria mmoja wa IT aliyejulikana kwa jina la Sandes Kazeze (22) mkazi wa Malawi kufariki dunia baada ya gari alilokuwa amepanda kuligonga loli.
 
Akizungumza na mtandao  wa www.matukiodaima.comofisini kwake Kamanda wa polisi mkoani Iringa ACP Ramadhani Mungi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 28 mei majira ya saa 12 za Alfajiri huko katika Kijiji cha Iramba barabara kuu ya Iringa – Mbeya wilaya ya Mufindi.
 
Kamanda Mungi alisema marehemu alikuwa amepanda gari aina ya Toyota Hiace yenye namba za usajili IT 0116 mali ya Davious Timeson wa Malawi lililokuwa likiendeshwa na Madilisto Tambala (34) aliigonga gari aina ya scania lenye namba za usajili T 181 ARC likiwa na Trella namba T 972 AGR mali ya Mikoani Traders iliyoko Dar Es Salaam iliyokuwa ikiendeshwa na Edwin Komba (29) mkazi wa Dar Es Salaam na kusababisha kifo cha abiria mmoja na wengine wawili kujeruhiwa.
Kamanda aliwataja majeruhi hao ni Madilisto Tambala pamoja na Peter Malunda wote ni wakazi wa Malawi ambao kwa sasa wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Ilembula na kusema chanzo cha tukio hilo ni mwendo kasi wa dereva.
 
Wakati huohuo, huko katika maeneo ya Mlima Chanagarawe barabara kuu ya Iringa – Mbeya wilayani Mufindi gari aina ya Mitsubishi Fuso yenye namba za usajili T 167 AVE mali ya Safina wa Makambako iliyokuwa ikiendeshwa na Jailet Kimbe (25) akitokea Dar es Salaam kuelekea 
 
Makambako aligongana na gari aina ya Scania lenye namba za usajili T 849 CHP lenye trella namba T 984 CNE mali ya Super star wa Dar es Salaam lililokuwa likiendeshwa na Hamad Mkubwa (47) na pia kuligonga gari jingine aina ya Scania lenye namba za usajili T 612 ASF lenye trella namba T 120 AFT mali ya Eawadhi kisha kuacha njia na kupinduka na kusababisha kifo cha tingo wa Mitsubishi Fuso aliyetambulika kwa jina la Noel Nyika (22) mkazi wa makambako.
 
Na katika tukio lingine, mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Simon Mlomo (80) mahabusu na mkazi wa Nyololo mwenye CC namba 20/2013 aliyekuwa anakabiliwa na tuhuma za mauaji amefariki dunia wakati akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Mufindi mkoani Iringa.
 
Mbali na matukio hayo ya vifo, Kamanda alisema watu wasiofahamika waliiba gari aina ya Toyota Carina yenye namba za usajili T 794 AYN lenye rangi nyeupe na thamani ya shilingi 6,000,000/= ambayo ni mali ya Edward Lucas (43) mkazi wa Kihesa.
 
Tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 28 mei na kusema gari hilo lilikutwa maeneo ya Mshindo likiwa limetelekezwa.
NA DIANA BISANGAO WA MATUKIO DAIMA.COM, IRINGA

MSANII WA BONGO MOVIE MAREHEMU RACHEL HAULE AAGWA DAR

$
0
0
01
 Picha ya Marehemu Sheila Leo Haule (Rachel) ikiwa pembeni ya Jeneza lake mchana wa leo wakati wa kuagwa kwa mwili wake,kwenye viwanja vya Leaders Club,Jijini Dar es Salaam.

 Baadhi ya Wacheza filamu hapa nchini,wakiwa pembeni ya Jeneza la Mpendwa wao Sheila Leo Haule (Rachel) aliefikwa na umauti hivi karibuni. 
 Bw. Saguda ambaye ndie alikuwa mchumba wa Marehemu akilia kwa uchungu huku akiliwazwa na nduguye.
 
Mwenyekiti wa Bongo Movie,Steven Nyerere akilia kwa
uchungu.
 Sehemu ya wacheza filamu wa Bongo Movie wakilia kwa uchuku kwa kuondokewa na Mwenzao,Marehemu Sheila Leo Haule (Rachel) wakati wa shughuli ya kuaga mwili wake iliyofanyika mchana wa leo kwenye viwanja vya Leaders Club,Jijini Dar es Salaam.

WATUHUMIWA WA MLIPUKO WA MABOMU JIJINI ARUSHA WAPANDISHWA KIZIMBANI

$
0
0
WATU 17 wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu Mkazi jijini Arusha, kujibu mashitaka 16 yakiwemo ya kuua kwa kutumia bomu,kutesa
binadamu na kusajili vijana na kuwapeleka nje ya nchi kufanya ugaidi.

Watu hao walifikishwa mahakamani hapo leo na kusomemewa shitaka hilo
mbele ya Hakimu Mkazi Mustafa Siama ambapo hawakutakiwa kujibu chochote
kutokana na kile kilichoelezwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa
kusikiliza kesi hiyo.


Watuhumiwa hao wanadaiwa kutenda tukio hilo Aprili 13,katika nyumba ya
kulala wageni na baa ya Arusha Night Park iliyopo Mianzini jijini
hapa,ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi juni 11 mwaka huu kwa
mtuhumiwa namba moja na namba nne na watuhumiwa wengine waliobaki kesi
yao itatajwa tena
juni 12

Katika tukio hilo la mlipuko huo wa bomu watu 14 walijeruhiwa vibaya
katika maeneo mbalimbali ya miili yao hali iliyopelekea mmoja wa
majeruhi hao aliyefahamika kwa jina la Sudi Ramadhani mkazi wa
Kaloleni jijini hapa kufariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika
hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru.


Akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Polisi Arusha,kabla
ya watuhumiwa hao kufikishwa mahakamani,Mkurugenzi wa Mashitaka ya Jinai nchini (DCI) Isaya Mngulu amesema kuwa mara tu baada ya kutokea kwa
tukio hilo, polisi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama
walianza upelelezi na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao.

Ameongeza kuwa pia siku hiyo hiyo ya tukio hilo la mlipuko wa bomu
katika baa ya Arusha Night Park muda mfupi baadae bomu lingine la
aina ileile liligundulika kutegwa katika baa ya Washington ya jijini
hapa ambapo bomu hilo liliondolewa katika eneo hilo bila kuleta
madhara .

"Aidha baadhi ya watuhumiwa hawa pia walibainika kuwa na mikakati ya
mashambulizaya namna hiikatika maeneo mengine na sehemu mbalimbali
hapa nchini ambazo ni taasisi za Serikali na sehemu zenye mikusanyiko
ya watu,ambapo pia wanajihusisha na uandaaji wa vijana kutoka mikoa
mbalimbali hapa nchini na kuwapeleka nchi za nje ili kujiunga na
makundi ya kiuhalifu"alisema Mkurugenzi huyo wa Mashitaka nchini.

Mkurugenzi huyo amesema kwamba upelelezi wa matukio haya bado
unaendelea ili kuwakamata watiliwa shaka wenginewaliobaki katika
matukio ya milipuko ya mabomu katika Kanisa Katoliki Olasitna uwanja
wa Soweto yaliyotokea mwaka jana jijini hapa na sehemu nyingine
nchini.


Ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la
polisi kwa lengo la kuwafichua wahalifu wa ndani na nje wa matukio
haya ya kihalifuna matukio mengine kwa lengo la kuvuruga amani na
utulivu wan chi.
Mmoja wa watuhumiwa hao akipakiwa kwenye Gari la Polisi tayari kwa Kupelekwa Mahakamani kusikiliza kesi yao.
Watuhumiwa wakiwa kwenye gari ya Polisi.

Article 4

$
0
0

KATIBU MKUU KIONGOZI AKUTANA NA NCHI WASHIRIKA WA MAENDELEO JIJINI DAR ES SALAAM LEO.

 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akibadilishana mawazo na mabalozi na wawakilishi wa nchi washirika wa maendeleo kabla ya  mkutano aliowaandalia leo Mei 30, 2014 katika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro hotel jijini Dar es salaam kuzungumzia  michango katika Kapu la Afya (Health Basket Fund) pamoja na mpango wa serikali wa kuiingiza sekta ya afya katika  kutekeleza Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN)
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa saba kutoka kushoto) akiwa katika mazungumzo  na mabalozi na wawakilishi wan chi washirika wa maendeleo katika mkutano aliowaandalia leo Mei 30, 2014 katika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro hotel jijini Dar es salaam kuzungumzia  michango katika Kapu la Afya (Health Basket Fund) pamoja na mpango wa serikali wa kuiingiza sekta ya afya katika  kutekeleza  Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN)

PICHA NA IKULU

WAFANYABIASHARA NDOGONDOGO MJINI NJOMBE WAHAHA KWA KUUZIA BAADA YA HALMASHAURI KUWAFUKUZA

$
0
0
Mmoja wa Wafanyabiashara Hao Akirejesha Biashara yake Katika Eneo Lililopigwa Marufuku Baada ya Kuficha Kwa Kuhofia Kukamatwa na Halmashauri.

Na Gabriel Kilamlya Njombe

Sakata la kuwaondoa wafanyabiashara katika maeneo yao ya kufanyiabiakazi mjini njombe limendelea kushika kasi licha ya bunge kuzuia wafanyabia katika sehemu mbalimbali za miji mpaka serikali Itakapo tenga maeneo kwaajili ya kufanyia shughuli zao.

Hali hiyo imejitokea Mapema leo baada ya wafanyabiashara wanaofanyia biashara zao katika Maeneo mbalimbali Likiwemo eneo la Roman Catholiki Mjini Njombe kujikuta katika wakati mgumu baada ya uongozi wa kata ya njombe mjini kwa kushirikiana na uongozi wa mitaa mbalimbali kuambatana na Askari Polisi na Migambo Kwa lengo la Kutaka Kuwaondoa Katika Maeneo Hayo.

Zoezi hilo Limekuwa likifanyika mara kwa mara lakini wafanyabiashara hao wamekuwa wakishindwa kutekeleza agizo la kuwataka wahame katika eneo hilo ambalo ni hatari kwa usalama wao kutokana na kushinda pembezoni mwa barabara kuu ya Njombe Songea wakijishughulisha na ujasiliamali  kwa kuuza vitu mbalimbali.

sakata hilo leo Imeonekana kuwa tishio kwa wafanyabiashara hao ambao wamesema Serikali imekuwa ikiwalazimisha kuhama katika maeneo hayo ilihali hakuna maeneo shirikishi katika masuala ya kibiashara wanakooneshwa.

Kutokana na Hali Hiyo Kituo hiki kimelazimika kuwatafuta baadhi ya viongozi wa ngazi ya mitaa na kata ili kutolea ufafanuzi huo ambao Afisa mtendaji wa Kata ya Njombe Mjini Bwana Bonasius Mwalongo Amesema Kuwa Kama Serikali Haiwezi kuwaacha katika Maeneo Hayo Waendelea kufanya biashara hizo kwani ni hatari katika maisha yao na wateja wao.

Bryson Lupenza ni Afisa mtendaji wa Mitaa ya Kwivaha,National Housing na Mgendala,Mitaa ambayo imekuwa katika sakata hilo Ambaye Amesema Kuwa Amekuwa Akitoa Elimu kwa Wafanyabiashara Hao Zaidi ya mara 20 Lakini Wamekuwa Wakishindwa kutii Agizo la kuhama Katika Maeneo Hayo.

Agrey Mtambo ni Diwani wa Kata ya Njombe Mjini Ambaye Amesema Kuwa Bado Hajapokea Malalamiko hayo Lakini Ataendelea Kushughulikia Kwani Serikali inawajibu wa Kuwahamisha taratibu Mara baada ya kuwaandalia Maeneo Rafiki Katika Biashara Zao.

Wakati Bunge la Bajeti likipitisha Makisio ya Bajeti Katika Wizara ya Viwanda na Biashara Liliitaka Serikali Kuwaacha Wafanyabiashara Hao hadi pale Serikali Itakapo watengea Maeneo ya Kazi Hiyo Lakini Bado Azimio Hilo Limeonekana Kuendelea Kukiukwa na Baadhi ya Viongozi wa Mitaa na Kata.

VIONGOZI NA WATENDAJI WAKUU WA TAASISI ZINAZOUNDA JUKWAA LA HAKI JINAI WAKUTANA MJINI BAGAMOYO KWA MKUTANO WA SIKU MBILI.

$
0
0
Habari katika Picha:Viongozi na Watendaji wakuu wa Taasisi zinazounda Jukwaa la  Haki Jinai wakiwa katika Picha ya pamoja,mara baada ya ufunguzi wa  Mkutano wa siku mbili. 

Mkutano huo umefunguliwa na Mkurugenzi Mkuu wa Uendeshaji wa Mashtaka (DPP) Dr E.Feleshi.Pamoja na mambo mengine mkutano huo utaangalia Haki za Watoto walio katika Mgongano na Sheria za Jinai.

Walio kaa Kwenye viti,wa kwanza kushoto ni Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) John C Minja, wa
pili kushoto ni Mkrugenzi wa Mashtaka (DPP) Dr.  E.Feleshi,wa tatuni IGP Ernesti Mangu. 

Mkutano huu unafanyika katika Hotel ya Millenium Sea Breeze Bagamoyo kwa siku mbili kuanzia tarehe 30 Mei, 2014.Na Mpiga Picha wa Magereza.

Uplands fm radio Wanakuletea tamasha la -UMOJA KWANZA 2014 KUANZA MAY 31 LUDEWA MKOANI NJOMBE

$
0
0

Kwa mwaka 2013 Ilikuwa Hivi

TAMASHA LA UMOJA KWANZA LA UPLANDS FM NJOMBE JANA LATISHA MBAYA.

wanafunzi toka shule ya viziwa Njombe wakisafisha jukwaa siku ya tamasha la Umoja kwanza



Ellymathew Kika Kulia Dj Phily Katikati na Hosea Ndangale Kushoto watangazaji wa Uplands Fm Radio Walivyotokelezea Kwenye Tamasha la UMOJA KWANZA njombe.





Kiungo Mshambuliaji wa Timu ya Uplands Fm Radio Aliyeipatia Ushindi Timu Hiyo Kwa Kufunga Gori Moja Dhidi ya Timu ya Watuma Salamu wa UPLANDS FM anaitwa Sunday Bavuga.

Endelea Kufuatilia Picha za Matukio hayo Hapo Chini
.













 WAFANYAKAZI WA UPLANDS FM RADIO STEREO BAADA YA KUTOKA NA USHINDI WA GORI MOJA KWA BILA DHIDI YA WADAU WA UMOJA WA WATUMA SALAAM






 MKURUGENZI WA KITUO CHA RADIO UPLANDS FRM STEREO NJOMBE JAMES THOMAS SWALE AKIZUNGUMZA NA WADAU NA WASANII WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA NA WA FILAMU




 
WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI VIZIWI WAKIONESHA BURUDANI KWA KUCHEZA NGOMA





 WAIGIZAJI  WA FILAMU KUTOKA   KIBENA ARTS  GROUP  TOKA MTAA WA KIBENA NJOMBE 





MSANII WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA CHA  BONGO FRAVER  NJOMBE mahela akifanya yake.









 WADAU NA MASHABIKI WA MUZIKI WAKIWA PAMOJA NA WADAU WA UMOJA WA WATUMA SALAAM WA UPLANDS FM WAKISHUHUDIA VIPAJI KATIKA UWAJA WA SABASABA

 ANAITWA ADDY Ng'ari AKITOKA NA NGOMA YAKE YA UA











 SARAKASI NAZO HAZIKUCHEZA MBALI VIPAJI MBALIMBALI VILIKUWA VIKIONESHWA




 B. ALONE  NI MSANII WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA MKOA WA NJOMBE AMBAE ALIKUBALIKA SANA NA WAKAZI WA MKOA WA NJOMBE AKITOKA NA KIBAO CHAKE KINACHO MTAMBULISHA NCHI NZIMA YA TANZANIA NA AFRIKA MASHARIKI CHA KOMBORELA

 MKURUGENZI WA KITUO CHA RADIO  UPLANDS FM STEREO  JAEMES THOMAS SWALE AMBAO NDIYO WAANDAAJI WA TAMASHA LA UMOJA KWANZA KWA MWAKA 2013



MSANII WA FILAMU NAE AKIONESHA UJUZI WAKE.. 

Ilikuwa ni mwezi Julai 6 mwaka 2013,sasa May 31,2014 Kufanyika Ludewa na Wilaya nyingine za Mkoa wa Njombe

BREAKING NYUZZZZZ........:

$
0
0

GEORGE TYSON HATUNAYE TENA,AFARIKI DUNIA AJALINI MKONI MOROGOROTAARIFA ZILIZOIFIKIWA GLOBU YA JAMII USIKU HUU,ZINAELEZA KUWA ALIEKUWA MUONGOZAJI WA FILAMU NA VIPINDI MBALI MBALI VYA TELEVISHENI HAPA NCHINI,GEORGE TYSON (PICHANI) AMEFARIKI DUNIA.

GEORGE TYSON AMEFIKWA NA MAUTI HAYO USIKU HUU BAADA YA KUPATA AJALI MBAYA SANA KUTOKANA NA GARI WALIOLOKUWA WAKISAFIRIA KUTOKA MKOANI DODOMA KUJA DAR ES SALAAM,WAKITOKEA KWENYE HAFLA YA KUADHIMISHA MIAKA MIWILI YA KIPINI CHA TELEVISHENI CHA THE MBONI SHOW,KUPINDUKA MARA KADHAA KUTOKANA NA KUPASUKA KWA MIPIRA MIWILI (MATAIRI) YA GARI HIYO AINA YA TOYOTA NOAH.

AJALI HIYO IMETOKEA MAJIRA YA SAA MOJA JIONI,ENEO LA GAIRO MKOANI MOROGORO.

NDANI YA GARI HILO KULIKUWA NA WATU NANE AMBAO NAO HALI ZAO NI MBAYA KUTOKANA NA KUUMIA MAENEO MBALI MBALI YA MIILI YAO NA KUKIMBIZWA HOSPITALI YA RUFAA YA MOROGORO KWA MATIBABU.

TUTAENDELEA KUPEANA TAARIFA KADRI ZITAKAVYOKUWA ZIKITUFIKIA.

Article 2

$
0
0

WAANDISHI WA HABARI WAASWA KUSHIRIKIANA NA TMF ILI KUPUNGUZA UTEGEMEZI WA MATANGAZO

DSC_0540
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa mradi wa mafunzo ya bure kwa waandishi wa habari kwenye maeneo matano, sekta ya uchimbaji, unyanyasaji wa kjinsia, kupamba na biashara ya madawa ya kulevya na kuzuia utumiaji wa madawa ya Kulevya kwa waandishi wa habari na utayarishaji na utengenezaji wa vipindi vya luninga na wanawake watangazaji jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma. kushoto kwake ni Msaidizi wa Mwakilishi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Idadi ya watu, Dorothy Temu –Usiri na Mkurugenzi wa Mfuko wa vyombo vya habari, Ernest Sungura.(Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).

Na Damas Makangale, MOblog Tanzania
WAANDISHI WA HABARI nchini wamehimizwa kushirikiana kwa karibu na Mfuko wa Vyombo vya Habari (TMF) ili kuacha kutegemea zaidi matangazo kwa sababu kuna weka taaluma yao rehani.

Akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa mradi wa kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari jinsi ya kuripoti mambo ya sekta ya uchimbaji, unyanyasaji wa kijinsia, kupamba na biashara ya madawa ya kulevya na kuzuia utumiaji wa madawa ya Kulevyana watayarishaji wa vipindi vya luninga, Waziri wa kazi na Ajira, Mhe, Gaudensia Kabaka amesema kwamba vyombo vya habari lazima vishirikiane na mfuko huo ili kuwa huru wakati wa kuripoti.

“kuendelea kutengemea matangazo kutoka kwenye makampuni mbalimbali ili kujiendesha kuna wafanya kutokuwa huru katika uandishi wetu na tasnia ya habari kwa ujumla,” amesema Kabaka.

Amesema mradi huo wa mafunzo ya bure kwa waandishi ni muhimu kwa taifa kwa sababu tatizo kubwa la ajira hasa kwa vijana na wanawake linachangia kwa kiasi kikubwa vijana wengi kujiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya.
DSC_0434
Baadhi ya wadau na wageni waalikwa wakimsikiliza mgeni rasmi hayupo pichani.

Kabaka aliongeza kuwa mafunzo haya yatakayotolewa kwa ufadhili wa TMF ni muhimu ili kuelimisha jamii madhara ya kuuza na kusambaza dawa za kulevya na matumizi yake yanavyoathiri kizazi na kizazi.
“kwa sasa nchi yetu ya Tanzania ni moja ya nchi zilizoathirika sana na matumizi ya dawa za kulevya na mbaya zaidi kutumika katika njia ya kusambaza madawa hayo hatari,”

“kwa mujibu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii tuna jumla ya watu 20,626 walioathirika na dawa za kulevya na kwa sasa wanapatiwa matibabu,” alisisitiza Kabaka. Amesema nchini matumizi ya dawa za kulevya kwa zaidi ni Bangi, Heroin, Mirungi na Cocaine na cha kutisha matumizi haya yanaathiri pia wanafunzi wa sekondari na shule za msingi nchini.
DSC_0515
Msaidizi wa Mwakilishi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Idadi ya watu(UNFPA), Dorothy Temu Usiri akitoa nasaha zake kwenye uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.

Kwa upande wake, Msaidizi wa Mwakilishi Mkazi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Idadi ya watu, Dorothy Temu-Usiri amesema kuwa kuongezeka kwa vitendo vya kikatili vya kijinsia na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi vimechochea kushirikiana na TMF kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari hapa nchini.

“kwa kuanzisha mafunzo haya ya bure kutasaidia waandishi wa habari kuandika kwa kina juu ya madhara ya matumizi ya dawa za kulevya ambazo ndio kichocheo cha ukatili wa kijinsia hasa kwa Wanawake,” amesema Usiri.

Usiri aliongeza kwamba nchini Tanzania idadi kubwa ya watu wenye nguvu ya kufanya kazi ni vijana kwahiyo ni muhimu jamii ya kimataifa kushirikiana na serikali na taasisi zingine ili kunusuru kundi hili muhimu kwenye nchi.
DSC_0423
Mkurugenzi wa TMF nchini, Ernest Sungura akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo wa mafunzo ya bure yanayofadhiliwa na mfuko wake ambapo amesema kwamba malipo madogo kwa wahariri na waandishi wa habari kunadidimiza taaluma ya uandishi wa habari pamoja na swala la kutokubobea katika sekta husika (Specialization).


DSC_0490
Wadau watakaoshiriki kwa ukaribu kwenye mradi huo wakitambulishwa kwa mgeni rasmi kutoka kushoto ni Dkt. Pilly Said kutoka kitengo cha madawa ya kulevya hospitali ya Mwananyamala, January Nzisi Mkuu wa Kitengo cha Mtandao Tume ya Kudhibiti Madawa ya kulevya, Geodfrey Nzowa, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi, kitengo cha Kupambana na Madawa ya Kulevya, Bi. Aida Teshe Kaimu Kamishina kutoka Tume ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya (DCC) na Florence Bahati Khambi Afisa Habari kutoka Tume ya Kudhibiti dawa za kulevya.
DSC_0458
Wadau mbalimbali na wageni waalikwa wakifuatilia yaliyojiri kwenye uzinduzi wa mradi wa mafunzo ya bure kwa waandishi wa habari kwenye maeneo matano, viwanda, jinsia, madawa ya kulevya, kuzuia madawa ya kulevya kwa waandishi wa habari na utayarishaji na utengenezaji wa vipindi vya luninga na wanawake watangazaji jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.
DSC_0498
Afisa Habari kutoka kitengo cha Umoja wa Mataifa cha Habari (UNIC), Stella Vuzo amesema kwamba mradi huo umekuja katika muda mwafaka kwa taifa la Tanzania kwa sababu takwimu za matumizi ya dawa za kulevya zinatisha kwa vijana ni lazima taasisi za ndani na jamii za kimataifa kushirikiana kupambana na janga hili.
DSC_0405
Pichani juu na chini ni sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo katika maeneo mbalimbali.
DSC_0406
DSC_0410
DSC_0395
DSC_0418
Afisa Habari kutoka kitengo cha Umoja wa Mataifa cha Habari (UNIC), Stella Vuzo (kulia) pamoja na Bw. Phillip Musiba kutoka UNIC.
DSC_0432
Afisa mafunzo wa TMF, Bi. Raziah Mwawanga akinakili mambo muhimu yaliyokuwa yakijiri wakati wa uzinduzi huo.
DSC_0414
Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA(Mstaafu) Ananilea Nkya (kushoto) na Mwandishi wa Habari Mkongwe Mama Eda Sanga (katikati) ambaye ni miongoni mwa mentors kwenye mradi huo. Kulia Sawiche Wamunza kutoka UNFPA.

Article 1

$
0
0

MATUKIO KATIKA PICHA TAMASHA LA UMOJA KWANZA LUDEWA NJOMBE




 WACHEZAJI WA TIMU YA UPLANDS FM RADI WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WACHEZAJI WA TIMU YA LUDEWA FC SIKU YA TAMASHA LA UMOJA KWANZA.
 HII NI TIMU YA LUDEWA FC WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA

 TIMU YA UPLANDS RADIO WACHEZAJI WAKE WAKIFANYA MAZOEZI KABLA YA KUINGIA UWANJANI

 LUDEWA FC WAKIFANYA MAZOEZI KABLA MCHEZO KUANZA
 ELMETHEW KIKA  WA UPANDE WA KUSHOTO NA WA KATIKATI AFISA HABARI MKOA WA NJOMBE ALIYEWAKILISHA MKUU WA MKOA WA NJOMBE KEPTAIN MSTAAFU ASERI MSANGI KATIKA KUUNGA MKONO JITIHANDA ZA KUPAMBANA NA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI NA WA KWANZA KUTOKA UPANDE WA KULIA NI KEPTAIN WA TIMU YA LUDEWA FC NICKSON MAHUNDI WAKIENDELEA KUANGALIA KANDANDA DHIDI YA UPLANDS NA LUDEWA FC


 TIMU ZOTE MBILI UPLANDS NA LUDEWA FC WAKIPEANA MIKONO KABLA YA KUANZA MECHI
 WASANII WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA BONGOFRAVER KUTOKA WILAYA YA LUDEWA WAKIFANYA MAONESHO KATIKA UWANJA WA BURUDANI KWENYE TAMASHA LA UMOJA KWANZA LILILOANDALIWA NA RADIO UPLANDS FM KWA KUSHIRIKIANA NA TAASISI BINAFSI NA SERIKALI YA MKOA WA NJOMBE KUPIGA VITA ONGEZEKO LA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI.
WA PILI KUTOKA UPANDE WA KULIA NI AFISA HABARI MKOA WA NJOMBE CHRISTOPHA AMBAE AMEKWENDA KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA NJOMBE.

Timu ya Ludewa fc imefanikiwa kuichabanga goli tatu kwa moja dhidi ya Uplands fc katika mchezo wa kirafiki uliochezwa katika uwanja wa Ludewa  mjini na kujinyakulia mbuzi aina ya beberu kwa ushindi huo.


Mbuzi huyo ambae aliandaliwa na  kampuni ya Uplands Radio kutoka Njombe mjini aliifanya timu ya Ludewa kuonesha kipaji chao katika kusakata kabumbu siku ya tamasha la Umoja kwanza lililoandaliwa na Uplands fm Radio kwa kushirikiana na serikali na taasisi mbalimbali.


Tamasha hilo lililenga kuhamasisha jamii kujikinga na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI amba lilibeba ujumbe usemao Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI NI Zero Ambalo linatarajia kuendelea tena katika wilaya ya Makete mkoani Njombe juma mosi ya hiki hii .






 WANANCHI WILAYA YA LUDEWA WAKIWA KATIKA KUSHUHUDIA WASANII MBALIMBALI WAKITUMBUIZA KWENYE TAMASHA LA UMOJA KWANZA WILAYANI HUMO









 HUYU NI MC WA TAMASHA LA UMOJA KWANZA  MAMA NYEUPE JINA LAKE HALISI PILI NYENJE
BURUDANI KALI TOKA KWA WASANII WA KUNDI LA KIBENA ARTS GROUP WAKIBURUDISHA UMATI WA WANANCHI WALIOFIKA ENEO LA TUKIO WILAYANI LUDEWA AMBALO LILIBEBA UJUMBE WA MAAMBUKIZI YA VIRUSI NI ZERO

Uplands fm radio kutoka Mkoa wa Njombe kwa kushirikiana na taasisi nyingene za binafsi na uongozi wa serikali  mkoa wa Njombe  imeandaa tamasha kubwa ambalo limelenga kuelimisha jamii mkoani humo juu ya kupambana na maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa kutembelea Wilaya zote za mkoa huo ambapo Jumamosi ya wiki iliyopita tamasha kubwa lilifanyika wilaya ya Ludewa.


Meneja wa kituo cha Radio Uplands fm Novatus Lyaluu amesema kuwa Tamasha hilo limeshilikisha wadau mbalimbali wakiwemo wadau  wa kupambana na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI Mkoa wa Njombe watu wa Kuhamasisha matumizi ya Kondom  PSI Na kwamba tamasha hilo linatarajia kuendelea tena jumamosi ya wiki hii wilayani Makete na baadae Wanging'ombe na Makambako kwa kila Juma mosi.

Article 0

$
0
0

TANZANIA YA KWANZA AFRIKA MASHARIKI KATIKA USAFIRI WA MABASI YAENDAYO KASI - PINDA

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda  amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi za kwanza katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kuingia kwenye ubia na sekta binafsi katika mradi mkubwa wa usafirishaji abiria.
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Juni 3, 2014) wakati akifungua Mkutano wa Majadiliano yenye lengo la kuutangaza mradi wa mabasi yaendayo kasi kwenye ukumbi wa Mlimani City. Mkutano huo wa siku mbili, utamalizika kesho (Jumatano, Juni 4, 2014).
Waziri Mkuu amesema kutèkelezwa kwa mradi huo kutatoa fursa za ubunifu utakaowezesha kupatikana kwa suluhisho la usafiri mijini na hasa kwenye miji inakua kwa kasi barani Afrika.
"Mbali ya kutoa huduma za hali ya juu, za haraka na ambazo siyo ghali kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, nia ya Serikali ni kuona mfumo mpya wa matumizi ya kadi kwenye mpango huu wa usafiri unatumika ipasavyo," alisema.
Alisema ni matumaini ya Serikali kwamba wadau kutoka sekta binafsi ambao ni wazawa na wa kutoka nje ya nchi watashiriki kwenye mradi huu ili uweze kuboresha matumizi ya kadi ambayo mtu hatatakiwa kulipia fedha taslimu akiwa ndani ya basi bali kutumia kadi anayoilipia kabla ya kuingia ndani ya basi husika.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano huo, Waziri Mkuu alisema Serikali iliamua kuanzisha mradi huo ili kupunguza msongamano wa magari kwenye barabara za Jiji la Dar es Salaam.
"Hii ni awamu ya kwanza ambayo inakaribia kukamilika na inaanzia Kimara hadi Kivukoni na itakuwa na matawi mawili ya Morocco na Karikoo. Mradi wote una awamu sita za ujenzi kuelekea maeneo tofauti ya Jiji," alisema.
Mbali na mradi huo wa mabasi yaendayo kasi, Serikali inaangalia uwezekano wa kutumia usafiri wa majini kwa kutumia boti kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo kama njia mojawapo ya kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es Salaam.
Vilevile tutaimarisha usafiri wa reli kama njia nyingie ya kupunguza tatizo hili. Dk. Mwakyembe (Waziri wa Uchukuzi) ameanza na sote tumeona ni jambo linalowezekana. Cha msingi ni kuimarisha tu usafiri huu, aliongeza Waziri Mkuu.
Mapema, akiwakaribisha wajumbe wa mkutano huo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Bibi Hawa Ghasia alisema Serikali imedhamiria kuhakikisha kuwa mradi huo unafanikiwa.
Pia alitumia fursa hiyo kuishukuru Benki ya Dunia ambayo alisema imetoa kiasi cha dola za Marekani milioni 200 kwa ajili ya kufadhili mradi huo.
Mkutano huo unawashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wa ndani na wa nje wanaotarajiwa kutoa huduma za mabasi makubwa na madogo, utoaji tiketi, ulinzi, usafi na huduma za maduka.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM.
JUMANNE, JUNI 3, 2014.
Viewing all 2276 articles
Browse latest View live