AFISA MTENDAJI WA KIJIJI CHA IMALINYI ATAKIWA KUKABIDHI OFISI KESHO JUMATANO 18 JUNE KUTOKANA NA TUHUMA ZA KUVUJA MALI ZA KIJIJI
huyu ni afisa mtendaji wa kijiji cha Imalinyi Milton Mgobasa ambae amekataliwa na wananchi  na kupewa uhamisho na hapa anawasomea wananchi hesabu za mapato na matumizi ndipo akabidhi ofisi ya kijiji hicho.
Wananchi wa kijiji cha Imalinyi Wilayani Wanging'ombe mkoani Njombe wamemsamehe afisa mtendaji wa kijiji hicho bwana Milton Mgobasa mapungufu yaliojitokeza katika taarifa yake ya hesabu za mapato na matumizi ambayo hayajasomwa kwa wananchi kwa takribani mwaka mmoja na kuwataka watendaji wengine kuwa makini na utendaji wao kazi.
Wakiongea kwenye mkutano wa hadhara wananchi hao wamesema kuwa kutokana na uongozi wa kijiji hicho kuonesha mapungufu katika taarifa zao za hesabu za mapato na matumizi  wamemuomba mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Wnging'ombe kuagiza wakaguzi wa vitabu vya watendaji wa vijiji kila baada ya miezi mitatu ili kubaini wa watendaji  wasiyo wadilifu kazini.
Aidha wananchi hao wameitupia lawama ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri hiyo kwa kile kilichoelezwa na afisa mtendaji wa kijiji hicho Milton Mgobasa kwamba  ofisi ya mkurugenzi haina vitabu vya stakabadhi za michango ya maendeleo ya vijiji jambo ambalo diwani wa kata hiyo bwana Enock Kiswaga amekanusha hoja hizo za kukosekana vitabu.
WANANCHI WA KIJIJI CHA IMALINYI WAKISIKILIZA MAPATO NA MATUMIZI YA KIJIJI HICHO
MWENYEKITI WA KIJIJI CHA IMALINYI ADAM CHENGULA AKIZUNGUMZA NA WANANCHI
RISITI FEKI ALIZOKUWA AKIZITUMIA AFISA MTENDAJI HUYO NA HIZO NDIZO ZILIZO MUONDOA KIJIJINI HAPODIWANI WA KATA YA IMALINYI ENOCK KISWAGA AKIKANUSHA HOJA YA KUKOSEKANA KWA VITABU VYA STAKABADHI ZA VIJIJIÂ AMBAZO VIONGOZI WA VIJIJI WALIKUWA WAKIJITETEA KWAMBA OFISI YA MKURUGENZI HAINA VITABU VYA STAKABAZI HIZO
MGANGA WA ZAHANATI YA IMALINYI AKITOA MATANGAZO JUU YA KUPATIWA VITAMBULISHOÂ VYA MATIBABU BURE KWA WAZEE.
Â
Na Michael Ngilangwa Wanging'ombe
Wananchi wa kijiji cha Imalinyi Wilayani Wanging'ombe mkoani Njombe wamemsamehe afisa mtendaji wa kijiji hicho bwana Milton Mgobasa mapungufu yaliojitokeza katika taarifa yake ya hesabu za mapato na matumizi ambayo hayajasomwa kwa wananchi kwa takribani mwaka mmoja na kuwataka watendaji wengine kuwa makini na utendaji wao kazi.
Wakiongea kwenye mkutano wa hadhara wananchi hao wamesema kuwa kutokana na uongozi wa kijiji hicho kuonesha mapungufu katika taarifa zao za hesabu za mapato na matumizi  wamemuomba mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Wnging'ombe kuagiza wakaguzi wa vitabu vya watendaji wa vijiji kila baada ya miezi mitatu ili kubaini wa watendaji  wasiyo wadilifu kazini.
Aidha wananchi hao wameitupia lawama ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri hiyo kwa kile kilichoelezwa na afisa mtendaji wa kijiji hicho Milton Mgobasa kwamba  ofisi ya mkurugenzi haina vitabu vya stakabadhi za michango ya maendeleo ya vijiji jambo ambalo diwani wa kata hiyo bwana Enock Kiswaga amekanusha hoja hizo za kukosekana vitabu.
Akizungumza wakati wa kusoma hesabu ya taarifa ya mapato na matumizi afisa mtendaji wa kijiji cha Imalinyi ambae amepata uhamisho baada ya wananchi kumkataa Milton Mgobasa amesema kuwa kukosekana kwa vitabu vya stakabadhi za michango ya maendeleo ya miradi ya wananchi imesababisha kununua vitabu ambavyo halmashauri haijaidhinisha ili wananchi waendelee kuchangia miradi pasipo kutambua kuwa ni kinyume na sheria.
Diwani wa kata ya Imalinyi Enock Kiswaga amesema  marufuku kwa maafisa watendaji kununua kitabu mahala anapojua yeye na kuanza kukitumia pasipo halmashauri kuidhinisha huku akisema utetezi wa mwenyekiti wa kijiji hicho Adam Chengula na afisa mtendaji huyo kwamba halmashauri haina vitabu si wa kweli kwani vitabu halmashauri vipo vya kutosha na kwamba ni uzembe wa kuvifuata huku akitumia fursa hiyo kumtambulisha afisa mtendaji aliyehamia badala ya aliyekuwepo awali.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho bwana Adamu Chengula akiwa kwenye mkutano huo alikuwa mstali wa mbele kuwambia wananchi kuwa halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe haina vitabu vya stakabadhi kutokana na taarifa alizodai kuzipata kwa afisa taarafa wa Imalinyi jambo ambalo diwani wa kata hiyo alikanusha kauli hiyo.