Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Article 1

$
0
0

Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum awasilisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2014/15

 *Serikali kutumia trioni 19.853.3 *Bei ya Vileo kupanda*Ya Pembejeo kushuka*Wafanyakazi wapata nafuu ya kodi
Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum, akionesha mkomba wenye Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2014/15, nje ya viwanja vya Bunge wakati akielekea kwenye ukumbi wa Bunge kwa ajili ya kuiwasilisha leo, mjini Dodoma.

Na mwandishi wetu, Dodoma
WAZIRI wa Fedha, Saada Mkuya Salum, leo amewasilisha Bajeti ya sh. trioni 19.853.3 kwa ajili ya matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2014/2015, huku lengo likiwa kuongeza makusanyo ya mapato kwa kuanzisha vyanzo vipya, kuboresha vilivyopo na kupunguza misamaha ya kodi.
Waziri wa Fedha, Saada Mkuya ameliambia Bunge kuwa bajeti hiyo imelenga kupunguza gharama za maisha ya wananchi kwa kuendelea na jitihada za kudhibiti mfumuko wa bei, kuendelea kuboresha huduma za jamii na kuboresha miundombinu ikiwemo ya barabara na umeme.
“Aidha bajeti hii imezingatia pia maandalizi ya Katiba mpya, uchaguzi wa Serikali za Mitaa na maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015,”alisema Mkuya.
Waziri huyo alibainisha pia bajeti hiyo, imelenga kuongeza upatikanaji wa nishati ya umeme wa uhakika, kuboresha elimu, kuunganisha nchi kwa njia ya miundombinu ya barabara, reli na viwanja vya ndege.
Waziri huyo wa Fedha alisema Serikali imepanga kushughulikia kwa nguvu zaidi kero mbalimbali zinazowakabili wananchi zikiwemo upatikanaji wa maji, nishati ya uhakika, elimu kuhusu umuhimu wa faida za kulipa kodi kwa kutumia mitandao ya kieletroniki na kusiamia ulipaji kodi kwa hiari kupitia udhibiti wa matumizi ya mfumo wa mashine za kieletroniki za kutoa risiti ambao umeboreshwa zaidi.
Aidha, alisema ili kuleta ufanisi katika usimamizi wa bajeti, Serikali inaandaa muswada wa sheria ya bajeti ambao utaletwa bungeni mwaka huu.
Alisema katika kipindi hicho bajeti hiyo itatekeleza utoaji wa fedha kwa mafungu utakaozingatia uwasilishaji wa taarifa za matumizi ya kawaida na maendeleo kwa kila robo ya mwaka sanjari na kuwianisha pamoja na kuandaa sheria ya bajeti.
Aidha alisema mgawanyo wa fedha katika bajeti hiyo umewekewe kipaumbele katika sekta ya nishati na madini ambapo imetengewa asilimia 7 ya bajeti yote ya Serikali.
Kipaumbele kingine kimekwenda katika sekta ya miundombinu ya usafirishaji ambapo imetengewa sh. trioni 2.10 ambapo sh. bilioni 179 ni kwa ajili ya ununuzi wa mabehewa na ukarabati wa reli ya kati na nyingine huku trioni 1.414 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa barabara na madaraja.
“Azma hii inalenga kupunguza msongamano wa magari mijini, gharama za usafiri na usafirishaji wa bidhaa na huduma na hivyo kupunguza mfumuko wa bei,”alisema.
Mkuya alisema sekta nyingine iliyopewa kipaumbele katika bajeti hiyo ni kilimo ambapo sh. trioni 1.084 zimetengwa kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya umwagiliaji katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya SAGCOT, ujenzi wa maghala na masoko.
Hali kadhalika Elimu nayo imetengewa asilimia 23 ya bajeti ya Serikali ambapo vipaumbele vimewekwa katika kuimarisha ubora wa elimu ikijumuisha miundombinu ya elimu hatua ambayo itasaidia upatikanaji wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia sanjari na kuimarisha ikiwemo ni pamoja kujenga madarasa na maabara.
Alisema ili kuhakikisha vijana nchini wanapata fursa za ajira, juhudi zitawekwa kwenye kuimarisha vyuo vya ufundi stadi (Veta).
Maeneo mengine ni maji, afya na utawala bora ambapo Serikali imetenga sh. bilioni 579.4 kwa ajili ya kuimarisha utawala bora ikijumuisha kugharamia Bunge Maalum la Katiba, vitambulisho ya taifa, uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2014, kuhuisha daftari la wapiga kura, maandalizi ya uchaguzi mkuu mwakani na mapambano dhidi ya rushwa.
Aidha ili kuongeza mapato ya Serikali na kufikia malengo ya kiuchumi katika mwaka 2014/2015 wizara hiyo imependekeza kufanyiwa marekebisho ya mfumo wa kodi na tozoikiwemo kurekebisha kodi chini ya sheria mbalimbali na pia taratibu za ukusanyaji na usimamizi wa mapato ya Serikali.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles