Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Article 19

$
0
0







Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Mbeya Leonard Magacha(katikati) akiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA(kulia) wakati wa semina ya siku moja kwa wanahabari 120 wa mikoa 6 ya Nyanda za Juu Kusini leo asubuhi.

Baadhi ya waandishi wa habari kutoka mikoa 6 ya Nyanda za Juu Kusini wakiwa katika semina ya siku moja ya TFDA







Meneja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA kanda Rodney Alananga akifafanua jambo wakati wa semina iliyowahusisha wanahabari 120 kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

Shirika la Afya Duniani WHO Limebaini Kuwepo Kwa Ukiukwaji Mkubwa kwa baadhi ya wafanyabiashara wasiowaaminifu ambao Wamekuwa wakitengeneza Madawa feki na kuhatarisha Maisha ya Wananchi.

Akizungumza wakati wa Semina ya Wahariri na Waandishi wa Habari wa Nyanda za Juu Kusini Leo Jijini Mbeya Meneja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA Kanda ya Mashariki Bwana Emmanuel Alfonce Amesema Kuwa Kwa Mujibu wa Takwimu za WHO kwa mwaka 2006 Zimeeleza Kuwa Tanzania Imekuwa na Asilimia kumi ya Biashara ya Dawa Duniani kwa Hasara ya Dola za kimarekani bilioni 500 Kutokana na Madawa Feki.

Bwana Alfonce Amesema Kuwa Baadhi ya watanzania wasio waaminifu wamekuwa wakijishughulisha na utengenezaji wa madawa feki kama vipodozi pamoja na madawa ya Hospitali kitu kinachosababisha madhara makuwa kwa walaji.

Aidha Mamlaka Hiyo ya TFDA Imewataka wanahabari Kuendelea Kusema Ukweli juu ya Vyakula  Madawa Feki ambayo yamekuwa Yakiendelea Kusambazwa Kwa Wananchi Ili Kulinda Afya za Walaji.

Kauli Hiyo Imetolewa na Mwanasheria wa Mamlaka Hiyo Bwana Iskari Fute Wakati Akitoa Semina ya Siku  moja kwa Wahariri na Waandishi wa Habari wa Nyanda za Juu Kusini Iliyofanyika Jijini Mbeya.

Awali akifungua Semina hiyo Kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya,Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa huo Bwana Leonard Magacha Amesema Kuwa Kutokana na Jamii Kuamini Kila Kinachotangazwa na Vyombo vya Habari Hivyo Wanahabari Hawanabudi Kufanya Uchunguzi wa Kina na Kubaini Ukweli wa Kila Habari Kabla ya Kuitangaza.

Aidha Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA Imefanikiwa Kufungua Ofisi Nyingine Tano Katika Mikoa Tofauti Pamoja na Kufungua Maabara Kubwa yenye Kiwango cha Kimataifa Kwa ajili ya Kusogeza huduma karibu na Wananchi badala ya kubaki Dar es salaam.

Akizungumzia suala hili Kaimu mkurugenzi wa Mamlaka hiyo bwana Chrispin Severe amesema kuwa pamoja na kufanikiwa kufungua ofisi hizo na Maabara lakini bado mamlaka imekuwa inakabiliwa na changamoto mbalimbali katika kupambana na wafayabiashara wasiowaaminifu.

Amesema matarajio ni kuendelea kusimamia Viwango vya ubora wa bidhaa,kuwaelimisha wananchi kupitia waandishi wa Habari hapa Nchini.

Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa usalama wa chakula bwana Justin Makisi amesema kuwa endapo mamlaka hiyo haitosimama vizuri katika kudhibiti matangazo ya biashara ambazo si halali na hazina ubora basi jamii itapata madhara makubwa na hata kusababisha vifo kutokana na kutumia madawa na vyakula vilivyokwisha muda wake.

Amesema kuwa kama mamlaka tayari imefanikiwa kupiga marufuku na kuyafungia baadhi ya matangazo yaliyoonekana kupotosha umma ikiwemo dawa ya asili ya Fiterawa inayodaiwa kutibu ugonjwa wa vidonda vya tumbo.

Katika hatua nyingine amevitaka vyombo vya habari kutumia nguvu kubwa katika kuendelea kutoa habari na matangazo yanayopotosha umma katika maeneo mbalimbali ili jamii iweze kufahamu na kuepukana nayo.

Akizungumzia juu ya kushuka kwa ubora wa vyakula na Dawa mkurugenzi mkuu wa Maabara  Bi.Charys  Ugullum amesema kuwa kama maabara imekuwa ikifanya uchunguzi wa chakula,dawa na vidozi ili kubaini ubora na usalama wa bidhaa husika ili ziweze kuingizwa sokoni.

Ameongeza kuwa uchunguzi huo ukishafanyika unasaidia katika utoaji wa maamuzi juu ya chakula,dawa na vipodozi ambavyo vitabainika kuwa vina ubora au havina.

Amesema jumla ya sampuli 7546 za vyakula zimeshafanyika pamoja na vipodozi tangu kuanzishwa kwa mamlaka hiyo mnamo mwaka 2003.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles