Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Article 0

$
0
0
AUAWA KWA WIZI WA NG'OMBE MKOANI MBEYA 
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA AHMED MSANGI

 Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya Limethibitisha Kutokea Kwa Kifo cha Mkazi Mmoja wa Wilaya ya Momba Aliyeuawa Kwa Tuhuma za Wizi wa Mifugo.

Tukio Hilo Limemkumba Mtu Mmoja Aliyefahamika Kwa Jina La Amani Greyson Mwenye Umri wa Miaka 22  Mkazi Wa Iporoto Ameuawa Na Wananchi Walioamua Kujichukulia Sheria Mikononi Baada Ya Kumtuhumu Kuiba Ng’ombe Mmoja Mali Ya Babu Yake Aitwaye Geofrey Salamu.

Taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya Imeeleza Kuwa Tukio Hilo Limetokea Mnamo Tarehe 20.04.2014 Majira Ya Saa Nane Mchana Huko Katika Kitongoji Cha Maona, Kijiji Cha Twinzi, Kata Ya Bara, Tarafa Ya Itaka, Wilaya Ya Mbozi, Mkoa Wa Mbeya.

Imedaiwa Kuwa Marehemu Huyo Alikamatwa Na Askari Mgambo Na Kuwekwa Ndani. 


Aidha Imedaiwa  Kuwa Marehemu Alivunja Mlango Na Kisha Kuanza Kukimbi Na
Ndipo Wananchi Walimuona Na Kumshambulia.

Tarifa ya Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya Iliyosainiwa na Kamanda wa Polisi Mkoani Humo

Ahmed Msangi Imeeleza Kuwa Mwili Wa Marehemu Umehifadhiwa Katika Hospitali Ya

Wilaya - Vwawa Huku  Juhudi Za Kuwatafuta Waliohusika Na Tukio Hilo Zinaendelea.

Hata Hivyo Kamanda Msangi Ametoa Wito Kwa Jamii Kuacha Tabia Ya Kujichukulia Sheria

Mkononi Na Badala Yake Wawafikishe Watuhumiwa Wanaowakamata Kwa Tuhuma

Mbalimbali Katika Mamlaka Husika Kwa Hatua Zaidi Za Kisheria.

 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles