Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Article 0

$
0
0
 Lori Lililotolewa Plate Namba Yake na Anayedaiwa Kuwa ni Mkuu wa Kituo cha Polisi Njombe Baada ya Mhusika Kutopatikana Kwenye Gari Hilo Wakati wa Msako Huo.


 Malori Yenye Viazi Kwa Mtindo wa Lumbesa Yakitozwa Faini ya Shilingi Elfu Hamsini Kila Moja


 Hawa ni Baadhi ya Madalali wa Viazi Wakibishana Baada ya Mwenzao Mmoja Aliyefahamika Kwa Jina Moja la Good Kupigwa Pingu na Kupelekwa Kituo cha Polisi Kwa Tuhuma za Majibizano na Polisi.
 Hili ni Lori la Viazi Lililotolewa Plate Namba za Mbele Baada ya Mmiliki Kutokomea Kusiko Julikana Wakati Askari Polisi Wakitaka Kumtoza Faini Kwa Kununua Viazi Kwa Mtindo wa Lumbesa Leo

Na Gabriel Kilamlya Njombe.

Serikali Wilayani Njombe Imeenza Kuchukua Hatua Kwa Wafanyabiashara na Madalali wa Viazi Mviringo Wanaoendelea Kukiuka Agizo la Kununua Viazi Kwa Mtindo wa Zipu.

Hivi Karibuni Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba Alipiga Marufuku Ununuzi wa Viazi Kwa Mtindo wa Lumbesa Agizo Ambalo Limeonekana Kuendelea Kukiukwa.

Mchana wa Leo Wafanyabiashara Wanne wa Viazi Waliokiuka Agizo Hilo Wamejikuta Wakipigwa Faini Kutokana na Madalali Wao Kununua Viazi Kwa Mtindo wa

Lumbesa Huku Mmoja wa Madalali Akishikiliwa na Jeshi la Polisi Kwa Kile Kinachodaiwa Kujibizana Vibaya na Askari Polisi Waliokuwa Wakikamata Magari Hayo.

Wakizungumza na Kituo Hiki Mjini Njombe Mara Baada ya Kukamatwa na Jeshi la Polisi Kwa Kushirikiana na Ofisi ya Kata ya Njombe Mjini Baadhi ya Madereva Hao Wamesema Wao Hawapingi Agizo Hilo Lakini Serikali Bado Inashindwa Kudhibiti Tatizo Hilo Katika Maeneo Yote Huku Wakilalamikia Kitendo cha Mwenzao Mmoja Aliyefahamika Kwa Jina Moja La Good Kukamatwa na Jeshi laPolisi.

Wamesema Kuwa Pamoja na Wao Kutakiwa Kununua Kwa Mtindo wa Zipu Lakini Bado Hali Ya Soko Inaendelea Kuwa Ngumu Hususani Katika Soko la Dar es Salaam Kwani Baadhi ya Wafanyabiashara Kutoka Mikoa Mingine Wanaendelea Kuuza Kwa Mtindo wa Lumbesa na Kusababisha Viazi Vyao Kuharibika.

Akizungumza Mara Baada ya Kuwatoza Faini Hiyo ya Shilingi Elfu Hamsini Kila Gari Afisa Mtendaji wa Kata ya Njombe Mjini Bwana Donald Mng'ong'o Ameendelea Kuwataka Viongozi wa Ngazi za Chini Toka Vijijini Kuhakikisha Wanasaidiana na Wakulima Kupiga Vita Ununuzi wa Viazi Kwa Mtindo wa Lumbesa.

Bwana Mng'ong'o Amesema Kuwa Endapo Viongozi wa Chini Vinakotoka Viazi Hivyo Hawatofanya Kazi Hiyo Basi Wataendelea Kuongeza Ugumu wa Kazi Hiyo Kwa Baadhi ya Watendaji Wanaofanya Kazi Ya Kudhibiti Lumbesa.

Six  George Lupenza ni Katibu wa Chama cha Kuzuia Ununuzi  Viazi  Kwa Mtindo wa Lumbesa Mkoani Njombe Ambaye Amesema Licha ya Wao Kuendelea Kusaidiana na Serikali Kupiga Marufuku Biashara ya Viazi Kwa Mtindo wa Lumbesa Lakini Baadhi ya Madereva na Madalala Wanaendelea Kukiuka Agizo Hilo Jambo Ambalo Halitoweza Kuvumiliwa.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles