Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Article 2

$
0
0
WATU WAWILI WAMEFARIKI DUNIA MKOANI IRINGA





Watu Wawili Wafariki Dunia Mkoani Iringa Katika Matukio Mawili Tofauti, Likiwemo La Mtu Mmoja Aliyefahamika Kwa Jina La Niko Kilienyi (45) Kufariki Dunia Akiwa Anakimbia Mvua Isimnyeshee.

Akizungumza Na Mtandao wa Www.Matukiodaima.Com unaomilikiwa na Francis Godwin Ofisini Kwake Kaimu Kamanda Wa Polisi Mkoani Iringa ACP Wankyo Nyigesa Alithibitisha Kutokea Kwa Tukio Hilo Lililotokea Mnamo Tarehe 18 Machi Majira Ya Saa 11 Kamili Jioni Huko Maeneo Ya Kihesa Manispaa Ya Iringa.

Kamanda Wankyo Alisema Marehemu Alifariki Dunia Baada Ya Kuanguka Chini Wakati Akikimbia Ili
Mvua Isimnyeshee Hata Hivyo Chanzo Bado Kinachunguzwa.

Na Katika Tukio Lingine Mtu Mmoja Afariki Dunia Wakati Akipatiwa Matibabu Katika Hospitali Ya Tosamaganga Baada Ya Kugongwa Na Gari La Mizigo Huko Maeneo Ya Tanangozi Barabara Kuu Ya Iringa - Mbeya Iliyopo Katika Manispaa Ya Iringa.

Kamanda Alisema Tukio Hilo Lilitokea Mnamo Tarehe 17 Machi Majira Ya Saa 7 Kamili Mchana Ambapo Gari Lisilofahamika Aina, Namba Za Usajili Wala Dereva Lilimkanyaga Mpanda Baiskeli Aliyefahamika Kwa Jina La Clay Nzulumi (17) Ambaye Alikuwa Amedandia Ubavuni Mwa Gari Hilo.

Hata Hivyo Marehemu Huyo Alikimbizwa Hospitalini Kwa Ajili Ya Matibabu Ambapo Tarehe 18 Majira Ya Saa 6 Kamili Mchana Alifariki Dunia, Dereva Anatafutwa Kwa Sasa.



Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles