Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA

$
0
0

MBEYA

Mtu Mmoja Aliyefahamika Kwa Jina La William Henard Mwenye Umri wa Miaka 48 Mkazi Wa Magogo

Aliuawa Kwa Kukatwa Panga Kichwani Na Mbozyo Samson Mwenye Umri wa Miaka 40 Mkazi Wa Magogo.

Tukio Hilo Lilitokea Mnamo Tarehe 22.02.2014 Majira Ya Saa 23:30hrs Usiku Huko Katika Kitongoji Cha

Magogo Kijiji Cha Ileya, Kata Ya Ifwenkenya Tarafa Ya Songwe Wilaya Ya Chunya.

Chanzo Cha Mauaji Ni Wivu Wa Kimapenzi Kumgombea Regina Charles Mwenye Umri wa Miaka 39 Mkazi

Wa Magogo.

Mtuhumiwa Amekamatwa Na Taratibu Za Kisheria Zinaendelea Dhidi Yake.

Kaimu Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Mbeya Kamishina Msaidizi Wa Polisi
Robert Mayala Anatoa Wito Kwa Jamii Kutatua Migogoro Yao Ya Kimapenzi Kwa Njia Ya Kukaa Meza Ya

Mazungumzo.

Aidha Anatoa Wito Kwa Wapenzi Kuwa Waaminifu Kwa Kuwa Na Mpenzi Mmoja Ili Kuepuka Madhara

Yanayoweza Kuepukika.

Katika Tukio Jingine Mwendesha Pikipiki Aliyefahamika Kwa Jina La Danken Mwampashi Mwenye Umri wa

Miaka 42 Mkazi Wa Old  Vwawa Alifariki Dunia Baada Ya Kugongwa Na Gari Lenye  Namba Za Usajili It

6860 Aina Ya Toyota Corola Lililokuwa Likiendeshwa  Na Muulu Muulu Mwenye Umri wa Miaka 37 Raia Na

Mkazi Wa Ndola Nchini Zambia

Tukio Hilo Lilitokea Mnamo Tarehe 23.02.2014 Majira Ya Saa 09:00hrs Asubuhi Katika Barabara Ya
Mbeya/Tunduma Kijiji Cha Hanseketwa, Kata Ya Vwawa, Tarafa Ya Vwawa Wilaya Ya Mbozi.

Chanzo Cha Ajali Ni Mwendo Kasi Wa Mpanda Pikipiki Baada Ya Kuingia Barabara Kuu Bila Kuchukua

Tahadhali na Kwamba Mwili Wa Marehemu Umehifadhiwa Katika Hospitali Ya Serikali Ya Wilaya Ya Mbozi.

 Dereva Amekamatwa. Kaimu Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Mbeya Kamishina Msaidizi Wa Polisi
Robert Mayala Anatoa Wito Kwa Madereva Kuwa Makini Wanapotumia Vyombo Vya Moto Kwa

Kufuata/Kuzingatia Sheria Na Alama Za Usalama Barabarani Ili Kuepuka Ajali Zinazoweza Kuepukika.

Aidha Anatoa Wito Kwa Watumiaji Wengine Wa Barabara Kuzingatia Alama Za Usalama Barabarani Ili

Kuepuka Ajali Zinazoweza Kuepukika.
..............................................................................................................................................................................

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles