MSAFARA WA MGOMBEA UBUNGE CHADEMA KALENGA WAZUIWA NA POLISI IRINGA KWA MUDA.
Hapa polisi wakimtazama mgombea huyo akipita mbele yao |
Polisi Iringa wakiwa wameuzua msafara wa mgombea ubunge jimbo la Kalenga Bi Grace Tendega kupitia Chadema kwa madai hawakuwa na kibali cha kufanya maandamano hayo ya magari hapa ni eneo la lango la mji Samora ambapo msafara huo ulikuwa ukitokea maeneo la Ndiuka kuelekea kwa msimamizi wa uchaguzi ili kuchukua fomu ya NEC |
Mgombea ubunge wa Chadema kalenga Grace Tendega baada ya kuruhusiwa gari lake kupita |
Hapa polisi wakimtazama mgombea huyo akipita mbele yao |
|
Diwani Nyalusi kati akiwa chini ya ulinzi wa polisi |
Diwani wa Chadema kata ya Mvinjeni Iringa mjini Frank Nyalusi wa pili kushoto akiwa chini ya ulinzi wa polisi leo |
Viongozi wa Chadema Iringa wakiwa na mgombea wa ubunge jimbo la Kalenga katikati Bi Grace T Mvanga |
mgombea wa Chadema jimbo la Kalenga Grace T Mvanga akizungumza na wanahabari leo baada ya kuchukua fomu |
JESHI la polisi mkoani Iringa leo limeuzuia kwa muda msafara wa mgombea ubunge jimbo la Kalenga kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Grace Tendega Mvanga kwa madai kufanya maandamano yasiyo na kibali.
Huku Polisi hao wakimshikilia kwa muda diwani wa kata ya Mivinjeni Frank Nyalusi ( Chadema) kwa madai ya kuandaa mapokezi hayo bila kibali .
Tukio la kuzuiwa kwa mgombea huyo lilitokea mida ya saa 5 asubuhi wakati msafara wa mgombea huyo ukiwa na magari zaidi ya matano na pikipiki zaidi ya 20 ukikaribia kuingia Samora katika mji wa Iringa .
Hata hivyo mbali ya msafara huo kuzuiwa zaidi ya dakika 20 katika eneo hilo Mlima wa Ipogolo barabara kuu ya Iringa- Dodoma polisi waliweza kutumia busara zaidi ya kumruhusu mgombea wao kupita kuelekea kuchukua fomu huku wafuasi wengine wakizuiliwa kwa dakika tano na kuruhusiwa kumfuata mgombea wao ili kuufanya msafara huo kuwa katika hali ya kawaida na sio maandamano kama ilivyokuwa awali.
Pamoja na kuwaruhusu wafuasi hao ambao baadhi yao walianza kutoa lugha ya matusi kwa askari hao na kuwalazimisha kufyatua risasi jambo ambalo askari hao polisi hawakuweza kufanya hivyo wala kuwapiga mabomu ya machozi zaidi ya kumchukua kiongozi wao Frank Nyalusi kwa mahojiano zaidi.
Akizungumzia hatua ya polisi kuzuia msafara huo kwa muda katibu wa Chadema wilaya ya Iringa vijijini Felix Nyondo alisema kuwa wameshangazwa na hatua ya polisi kuzuia msafara huo kwani hayo hayakuwa maaandamano bali ni mgombea wao kutoka nyumbani kwenda kuchukua fomu kwa mujibu wa utaratibu wa msimamizi wa uchaguzi huo.
Nyondo alisema walivyofanya Chadema ni kama walivyofanya CCM wakati mgombea wao akienda kuchukua fomu ambapo CCM walikwenda mbali zaidi kwa kuwa na watu ambao walikuwa wakitembea kwa miguu na wao Chadema hawakufanya hivyo na badala yake walitumia magari na pikipiki kuelekea kwa msimamizi huyo.
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi alipotafutwa kwa njia ya simu na mtandao huu wa www.matukiodaima.com ili kuelezea zaidi hatua ya kuzuia msafara huo na kumshikilia kada huyo wa Chadema hakuweza kupatikana japo mmoja kati ya maofisa wa polisi waliokuwepo eneo la tukio alisikika akisema kuwa lengo la kuzuia msafara huo halikuwa lina ubaya ila ni katika polisi kutimiza wajibu wake wa kuhakikisha kila kitu kinafanyika kwa misingi ya sheria.
Kwani alisema Chadema walipaswa kuomba kibali kwa ajili ya kumpokea na kumsindikiza mgombea wao kuchukua fumu na polisi wangekuwepo kwa ajili ya kulinda usalama wao ikiwa ni pamoja na kuwaongoza njia ambavyo wangependa kupita ila sio hivyo walivyofanya kwa kutumia nguvu kusababisha msongamano wa magari katika barabara hiyo.
Kwa upande wake mgombea ubunge wa Chadema kalenga Bi Mvanga akizungumza na wanahabari alisema kuwa anawapongeza wana Chadema jimbo la kalenga kwa kuendelea kumuunga mkono na kuwa lengo la Chadema ni kuona wana Kalenga wanampata mrithi wa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo marehemu Dr Wiliam Mgimwa (CCM) mwenye uwezo wa kuwatumikia wananchi ambapo kwa upande wake anao uwezo huo.
Mgombea huyo alipongeza shughuli mbali mbali za kimaendeleo zilizofanywa na mbunge Dr Mgimwa kwa jimbo la kalenga na kuahidi kuendeleza jitihada hizo za kimaendeleo iwapo wananchi wa Kalenga watamchagua katika uchaguzi huo mdogo.
" Kuna mambo ambayo marehemu aliahidi na kuishia njiani katika kuyafanikisha na kuwa nafasi hiyo ataitumia kwa kufuatilia yote ambayo hayajafikia ukingoni "
Kuhusu msafara wake kuzuiwa na polisi alisema kuwa hizo ni changamoto za kuwaida katika kuelekea kwenye ukombozi wa kweli kwa wana kalenga kumpata kiongozi makini .
Zoezi la uchukuaji fomu la mgom bea huyo lilifanyika majira ya saa sita mchana katika ofisi za msimamizi wa uchaguzi Jimbo la KalengaPudenciana Kisaka ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halimashauri ya Iringa Vijijini.
Kisaka alimkabidhi fumo namba 8 mgombea huyo pamoja na nyaraka mbalimbali za Tume ya uchaguzi ikiwamo sheria za uchaguzi Kanuni za uchaguzi na pia katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na kumtaka mgombea kwenda kujisomea kwa lengo la kuongeza uelewa ili kuepusha vurugu wakati wa kampeni na uchaguzi wenyewe.
Kisaka aliwaambia waandishi wa habari kuwa hadi sasa ni wagombea wawili kutoka vyama vya CCM na Chadema pekee ndio wamejitokeza kuwania kiti cha Ubunge katika jimbo hilo huku akiongeza kuwa mwisho wa kurejesha fomu ni Februari 18 mwaka huu .
“Hadi sasa tunavyama viwili ambavyo wagombea wake wameshachukua fomu ya kuwania Ubunge kwa jimbo la Kalenga ,hata hivyo sheria bado inatoa Fursa kwa vyama kuendelea kujitokeza hadi kuchukua na kurejesha hadi leo kabla ya saa kumi jioni”alisema Kisaka.
Uchaguzi wa Kalenga unatarajia kufanyika Machi 16 mwaka huu na unalengo la kuziba pengo lililoachwa wazi na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Marehemu Dk Wiliam Mfimwa aliyefariki dunia Januari Mosi mwaka huu,katika uchaguzi huo CCM imemsimamisha Godfrey Mgimwa mmoja w awatoto w marehemu Mgimwa kupeperusha bendara ya chama hicho.
Grace T Mvanga alipata kugombea jimbo la Kalenga kwa mara ya kwanza mwaka 2005 kupitia Chama cha Jahazi Asilia na kushika nafasi ya pili kwa kura 13000 huku mgombea wa CCM kwa kipindi hicho George Mlawa akishinda kwa kishindo na bila kukata tamaa mwaka 2010 Grace T.Mvanda alijitokeza tena kugombea kupitia chama cha Jahazi Asilia na kushuka kwa kupata kura 3000 pekee huku mgombea wa CCM Dr Wiliam Mgimwa akiongoza na safari hii kuibukia Chadema ambao anagombea kwa mara ya kwanza kupitia Chadema na mara ya tatu katika Historia yake ya kuusaka ubunge Kalenga hivyo macho na masikio ya wengi kuona kama atapanda ama atazidi kushuka zaidi
Kwa hisani ya fg blog