Waziri wa Ujenzi,Dkt. John Pombe Magufuli Kesho Anatarajiwa Kuwa Mgeni Rasmi katika
hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa barabara itakayotekelezwa katika mikoa ya
Ruvuma na Mtwara.
Miradi hiyo itahusisha ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kati ya Namtumbo na
Tunduru ambayo imegawanywa katika sehemu tatu ambazo ni Namtumbo – Kilimasera
(km 68.20), Kilimasera – Matemanga (km 58.70) na Matemanga-Tunduru (km 60.70).
Tayari Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) ambayo inayofadhili ujenzi huo kwa
pamoja na Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), imetoa kibali kwa ujenzi wa sehemu
mbili za kuanzia Namtumbo hadi Kilimasera na Matemanga hadi Tunduru. Sehemu kati
ya Matemanga na Kilimasera itasubiri kibali kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika
ambacho pia kinatarajiwa kutoka hivi karibuni.
Hii ni mara ya pili kwa sehemu hiyo ya barabara kupata makandarasi. Awali kampuni ya
Progressive-Higleig Joint Venture kutoka India ndiyo iliyokuwa imeshinda zabuni hiyo
mwaka 2010 lakini baadaye ikasimamishwa kutokana na kushindwa kutimiza masharti
ya kimkataba na kuonyesha udhaifu katika utekelezaji wa mradi huo.
Katika hatua nyingine kesho pia utasainiwa mkataba wa ujenzi wa sehemu ya barabara
inayoanzia Mangaka mkoani Mtwara hadi Nakapanya (km 70.50) katika mkoa wa
Ruvuma. Vile vile utasainiwa mradi mwingine wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha
lami kuanzia Nakapanya hadi Tunduru (km 66.50) utakaotekelezwa mkoani Ruvuma.
Kusainiwa kwa miradi hii ni faraja kubwa kwa wakazi wa mkoa wa Ruvuma pamoja na
mikoa yote ya kusini kwani barabara hiyo ni kichocheo kikubwa kwa shughuli za
kiuchumi na kijamii katika maeneo hayo.
Hafla ya utiaji saini wa miradi hiyo itafanyika Kesho tarehe 17 Februari, 2013 katika Hoteli
ya Court Yard (Protea) Jijini Dar es Salaam Kuanzia saa 3:00 asubuhi.