MBEYA CITY1-1SIMBA FC
Mbeya City Yashindwa Kutamba Uwanja wa Nyumbani
Wachezaji wa Mbeya City Wakishangilia Gori Lao La Kwanza Lililofungwa Dakika ya 11 Kwa Mkwaju wa Penalt Kabla ya Simba Kusawazisha.![]()
Mvua Kubwa Yaanguka Wakati Mbeya City Ikimenyana na Simba Sports Club Katika Dimba la Sokoine Mbeya,Wachezaji wa Simba Wakishangilia Gori la Kusawazisha.![]()
Mbeya City Yashindwa Kutamba Uwanja wa Nyumbani
Na Emanuel Madafa
Mbeya city imishindwa kutamba katika uwanja wao wa nyumbani mara baada ya kukubali kugawana pointi Simba Spots Club ya jijini Dar es salaam kwa kutoka sare ya kufungana bao 1-1 Uwanja wa Sokoine Mbeya.
Hadi mapumziko, tayari Mbeya City walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililofungwa na Deogratius Julius kwa penalti dakika ya 13, akimchambua vizuri kipa Mghana, Yaw Berko.
Penalti hiyo ilitolewa kufuatia beki Joseph Owino kuunawa mpira katika harakati za kuokoa krosi ya Deus Kaseke kutoka wingi ya kushoto.
Mbeya City walitawala mchezo na kipindi cha kwanza na Simba SC ilimtumia Ramadhani Singano ‘Messi’ kushambulia, ambaye hata hivyo aliwekewa ulinzi mkali na mabeki wa timu ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya.
Mshambuliaji Mrundi Amisi Tambwe aliunganishia juu ya lango kwa kichwa mipira miwili ya adhabu iliyopigwa na Amri Kiemba kipindi cha kwanza, kufuatia Messi kuangushwa.
Kocha Mkuu wa Simba SC, Mcroatia Zdravko Logarusic kwa pamoja na wasaidizi wake Suleiman Matola na Iddi Pazi waliwafuata marefa katikati ua Uwanja kuwalalamikia
walikuwa wanawapendelea wenyeji na kuwaomba kipindi cha pili wachezeshe haki.
Kipindi cha pili, Simba SC ilibadilika mno na kuongeza kasi ya mashambulizi, hatimaye kufanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 50 mfungaji Mrundi Amisi Tambwe, aliyemalizia krosi ya Haroun Chanongo.
Baada ya Simba SC kusawazisha, kasi ya mchezo iliongezeka kwa pande zote mbili, timu zote zikishambuliana kwa zamu hadi mpira unakwisha.
Baada ya Simba SC kusawazisha, kasi ya mchezo iliongezeka kwa pande zote mbili, timu zote zikishambuliana kwa zamu hadi mpira unakwisha.
Matokeo hayo yanaifanya Mbeya itimize pointi 35 sawa na Yanga SC iliyo nafasi ya pili kwa wastani mzuri wa mabao wakati Simba inatimiza pointi 32 na inabaki nafasi ya nne.