MMOJA MBARONI KWA MAUAJI LUDEWA NJOMBE
Kamanda wa Polis Mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani
Na Michael Ngilangwa
Jeshi la polisi mkoa wa Njombe linamshikilia mkazi mmoja wa kijiji cha Madunda Wilayani Ludewa Samson Haule kwa tuhuma za kuhusika na mauaji yaliotokea katika kata ya Mawengi.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe Fulgence Ngonyani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa huyo anashikiliwa kwa mahojiano kutokana na tuhuma za kuhusika katika mauaji yaliomkuta Anna Solomon mwenye umri wa miaka 58 mkazi wa kijiji cha madunda Wilayani Ludewa.
Kamanda Ngonyani amesema kuwa tukio hilo limetokea mnamo february 11 mwaka huu majira ya saa kumi jioni ambapo marehemu akiwa amelala nyumbani kwake alivamiwa na
watu wasiyofahamika kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na kufariki dunia.
Amesema kuwa chanzo cha tukio hilo kinasadikika ni mgogoro wa mashamba ambao walikuwa wakigombania ambapo uchunguzi dhidi ya tukio hilo bado unaendelea na utakapokamilika mshtakiwa atafikishwa mahakamani.