Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Article 1

$
0
0
PINDI CHANA AWATAKA WANAWAKE LUDEWA KUENDELEA KUJIUNGA NA VIKUNDI ILI KUPATA MIKOPO.
Naibu Waziri wa Wanawake , Jinsia na Watoto Dkt. Pindi Chana Ameahidi Kushirikiana na Wanachi Mkoani Njombe Katika Shughuli Mbalimabli za Kiuchumi Pamoja na Kuhakikisha Wanawake Wanapata Mikopo ya Nafuu Kutoka Serikalini.

Naibu Waziri Chana Amesema Hayo Wakati Akizungumza na Wanachi wa Wilaya ya Ludewa na Kuongeza Kuwa Serikali Imekuwa  Ikiwapigania Wanawake na Vijana Ili Waweze Kujikwamua Kiuchumi na Kuleta Maendeleo ya Taifa Huku Akiwataka Wanawake Kuunda Vikundi Ama Kujiunga Kwenye Vikundi Ili Waweze Kupata Mikopo Hiyo Kwa Urahisi.

Ziara Hiyo ya Siku Mbili ya Naibu Waziri Mkoani Njombe Ililenga Kuzungumza na Wananchi wa Mkoa Huo Hususan Wanawake na Watoto Wakike Pamoja na Kutoa Shukrani Kwa Wananchi Hao Kwa Kumuwezesha Kuteuliwa Kuwa Naibu Waziri wa Wanawake , Jinsia na Watoto.

Awali Akizungumza Kwenye Mkutano Huo wa Hadhara Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Juma Solomon Madaha Amempongeza Dkt. Chana Kwa Kuteuliwa Kuwa Naibu Waziri wa Wanawake , Jinsia na Watoto Huku Akimuamba Naibu Waziri Huyo Kusaidia Idara ya Maendeleo ya Jamii Inapata Fedha Kwa Ajili ya Wanawake na Watoto na Kuongeza Kuwa ni Miongoni Mwa Idara Isiyokuwa na Bajeti ya Kutosha.

Mkuu Huyo wa Wilaya Ameongeza Kuwa Kuteuliwa Kwake Pia Kutasaidia Idara ya Maendeleo ya Jamii Kupata  Bajeti ya Kutosha Ili Wataalam wa Idara Hiyo Wanapata Mafungu ya Kuwafikia Wanawake na Watoto wa Kike Walioko Maeneo ya Vijijini Kwa Lengo la Kutoa Elimu Juu ya Haki Zao za Msingi.

Akizungumza mbele ya Naibu waziri huyo mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ludewa bwana Stanley Kolimba amewataka wananchi kuonesha ushirikiano kwa kiongozi huyo huku akisema zoezi la uundaji wa vikundi vya ujasiliamali linatakiwa kuendelezwa ili kujikwamu kiuchumi.

Hata hivyo ametaka wananchi kuondoa matabaka badala yake washikamane na washirikiane na viongozi wao wa Wilaya na kitaifa kwa ujumla ili kusukuma maendeleo ya Wilaya na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wao wanawake kutoka Wilaya ya Ludewa wameshukuru kwa Naibu waziri Dkt Pindi Chana kwa kufika katika Wilaya hiyo na kuwashukuru mbapo wamepongeza kwa uamuzi uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kwa kumteua Naibu Waziri huyo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles