Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

TAARIFATOKA POLISI MKOA WA DODOMA TAREHE 25.01.2014

$
0
0

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

    JESHI LA POLISI TANZANIA.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME ametoa tahadhari kwa
wananchi wa Mkoa wa Dodoma kuwa na tahadhari katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha maeneno mbalimbali.

Ametoa thahadhari hiyo baada ya kutokea tukio la PHILIPO SUNGURA, Miaka 55, Mgogo Mkazi wa Kijiji cha Mpinga Kata ya Kigwe WilayaniBahi kufa maji wakati akijaribu kuvuka mto Mpinga ambao ni wa msimu. Tukio hilo lilitokea tarehe 24.01.2014 majira ya saa 18:45 jioni wakati akijaribu kuvuka mto huo huku maji yakiwa ni mengi.
 
Kamanda Misime ameeleza imembidi kutoa tahadhari hiyo kwani kumbukumbu zinaonyesha watu wengi hupoteza maisha inapofika msimu wa mvua wakiwemo watoto wanaokwenda kuoga na kuchota maji katika mabwawa, mito ya msimu na madimbwi yaliyotuama maji kwa kunasa kwenye tope na kupoteza maisha.
 
Mfano anaeleza tangu mvua za msimu zilipoanza mwaka huu 2014 watu wanne (4) wameshapoteza maisha. Amewaomba Viongozi wa Mitaa, Vitongoji, Vijiji, Kata, Tarafa na waalimu mashuleni
kuwaeleimisha wananchi na wanafunzi ili kuepukana na matukio hayo.

          [DAVID A. MISIME - SACP]
 
KAMANDA WA POLISI MKOA WA DODOMA

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles