Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

HALI MBAYA TANZANIA

$
0
0
Wananchi wa Dumila mkoani Morogoro wakitumia uzoefu wao wa kuogelea kujinusuru na mafuriko yaliyotokea juzi na kuhatarisha maisha ya watu wengi ikiwa ni pamoja na kuharibu madaraja. 

Picha na Lilian Lucas  

Na Hamida Sharif na Lilian Lucas, Mwananchi
Maji yamejaa upande wa Kijiji cha Magole, kutokana na kukingwa na barabara mpya inayojengwa eneo hilo.


Dumila, Kilosa. Baadhi ya wananchi wa Dumila, Kilosa mkoani Morogoro ambao walikumbwa na mafuriko, wamesema maafa hayo yamewaacha watupu, kutokana na
kila walichokuwa nacho kusombwa na maji.
Waandishi wa Mwananchi walisema baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Magole ambacho kimeathiriwa kwa kiasi kikubwa na mafuriko hayo, nyuso zao zilionekana zikiwa zenye huzuni, huku baadhi yao wakiopoa vitu kutoka kwenye tope lililojaa katika nyumba zao.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye alitembelea eneo la maafa jana mchana, naye alionja chungu ya mafuriko hayo pale alipolazimika kuhutubia wananchi barabarani akiwa juu ya gari kutokana na maeneo mengine ya Kijiji cha Magole kujaa maji.
Mafuriko hayo yalisababisha mamia ya watu kupoteza makazi na mali, wakati Daraja la Mto Mkundi linalounganisha Wilaya za Kilosa na Mvomero lilivunjika na kukatisha mawasiliano kati ya mikoa ya Bara na Dar es Salaam.
Nyumba, miundombinu mbalimbali, majengo ya shule, taasisi za binafsi na serikali pamoja na mashamba viliharibiwa au/na kusombwa na maji hivyo kusababisha maelfu ya watu kukosa huduma muhimu kama vile vyakula, mavazi na malazi.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Magole, Koletha Mahululu alisema: “Tulipoona maji yanakuja kwa kwa kasi, tuliwatoa watoto wa darasa la kwanza hadi la tatu, kwani wengi wana umri mdogo mno.
“Uzuri wake hakuna madhara zaidi ya hasara kwani vifaa vya shule, madawati yamesombwa, vyoo vya shule na nyumba za walimu zimebomoka na nyingine kuharibika kabisa.
“Hapa tunasubiri taarifa ya Serikali ya mkoa kutuelekeza ni lini shule itafungwa na kufunguliwa kwa kuwa hakuna kinachoendelea,” alisema Mwalimu Mahululu.
Pinda na Dk Magufuli
Waziri Mkuu Pinda, akizungumza na wananchi hao alisema: “Nimeona uharibifu uliotokana na mafuriko, lakini baada ya kutafakari, Serikali imeanza kuleta vyakula, mavazi na huduma nyingine za maji safi ili kukabiliana na hili.”
Pinda alimwagiza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera kuhakikisha timu ya madaktari inaweka kambi katika eneo hilo ili kukabiliana na mlipuko wowote wa magonjwa endapo utajitokeza.
Aliahidi kwamba Serikali itahakikisha ujenzi wa Daraja la Magole ambalo sehemu kubwa ya udongo uliokuwa kwenye kingo zake, umezolewa na maji, linakamilika ndani ya siku nne zijazo, iwapo hakutatokea mafuriko mengine makubwa katika eneo hilo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles