Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Article 10

$
0
0

RAIS CATHERINE SAMBA-PANZI AAPISHWARAISI_ed66a.jpg

Mashahidi wanaripoti uporaji mkubwa wa mali katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, huku kaimu rais mpya akianza rasmi kazi yake.
Mwandishi wa VOA Nick Long amabye yuko mjini Bangui, ameiambia Sauti ya Amerika kuwa maelfu ya watu walipora mali katika eneo linalojulikana kama PK13 lenye wakazi wengi Waislam.
Anasema majeshi ya Rwanda yaliwafukuza waporaji, lakini uporaji ukaanza tena baada ya walinda amani hao wa
Rwanda kuondoka, kulinda sherehe za kuapishwa kwa kaimu rais mpya.
Rais huyo mpya wa muda Catherine Samba-Panza, ametoa mwito wa utulivu wiki hii kabla ya sherehe za kuapishwa kwake, ambako kumefanyika katika majengo ya bunge leo Alhamis
Chanzo, voaswahili.com (R.M).

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles