WAZIRI GEORGE MKUCHIKA AKIWA RCC NJOMBE ASEMA IDARA YA ELIMU YAONGOZA KWA RUSHWA MKOA WA NJOMBE.
Waziri George Mkuchika Akilalamikia Kushamiri Kwa Vitendo Vya Rushwa Nchini![]()
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Akizungumza Kwenye Kikao cha RCC Mkoa wa Njombe Leo.Wakuu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Njombe
Waziri Mkuchika Ataja Taasisi Vinara Kwa Rushwa Mkoa wa Njombe,Elimu Yaongoza.
Na Gabriel Kilamlya Njombe
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora George Mkuchika Amezitaka Halmashauri za Wilaya Mkoani Njombe Kuzitumia Kamati za Maadili Kwaajili ya Kudhibiti Vitendo Vya Rushwa na Kuimarisha Maadili Miongoni Mwa Watumishi wa Umma Hapa Nchini.
Aidha Serikali Imewataka Viongozi Mkoani Njombe Kuzingatia Dhana ya Utawala wa Sheria na Inayosimamia Katika Haki za Binadamu Ili Kuifanya Tanzania Kuendelea Kuwa Mahala Salama Zaidi Kuishi na Kuiwezesha Nchi Kuendelea Kuaminika Katika Jumuiya za Kimataifa.
Akizungumza Wakati wa Kikao Cha Kamati ya Ushauri Mkoa wa Njombe,Waziri Mkuchika Amesema Vitendo Vya Rushwa Haviwezi Kuisha Hapa Nchini Endapo Hkautakuwa na Watendaji Waadilifu na Viongozi Wenye Kutuhubutu Katika Kuchukua Hatua Dhidi ya Vitendo Vya Rushwa.
Amesema Endapo Kamati za Maadili Zitaundwa na Kutumika Vizuri Katika Halmashauri za WSilaya,Mapambano Dhidi ya Rushwa Yanaweza Kupata Nguvu Zaidi na Hivyo KUsaidia Kupunguza Kiwango Cha Rushwa Kinachosababisha Wananchi Kupoteza Imani na Serikali Yao.
Alisema katika mkoa wa Njombe pekee Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa miaka miwili iliyopita imepata taarifa za rushwa 116 na 80 kati ya hizo kufunguliwa majarada mahakamani, huku idara ya elimu ikiongoza kwa kuwa na taarifa 19 na majarada 12 ikifuatiwa na polisi yenye taarifa 18 na
majarada 12.
Akifafanua zaidi Mkuchikia alisema mabaraza ya ardhi ya kata yanashika nafasi ya tatu kwa kuwa na taarifa 9 majarada 5, afya taarifa 7 majarad 4, Tanesco taarifa 15, Mahakama taarifa 4 na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PSPF taarifa 1.
Alisema idara nyingine zinazotajwa kukithiri kwa rushwa ni Ardhi, Kilimo na Maji, na kutoa wito kwa viongozi kuzingatia maadili katika utumishi wao ili kutenda haki kwa wananchi.
"Niwazi kuwa rushwa ni kikwazo cha utawala bora, na ili kupamba na hali hii ni wazi kuwa kila mtumishi azingatie maadili," alisema Mkuchika.
Alisema kama mapambano dhidi ya rushwa yataendelea kushamiri nchini ni dhahiri kwambwa hata mataifa makubwa hayawezi kuipa ruzuku Tanzania.
Kwa Upande Wake Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Njombe Bw Charles Nakembetwa Amesema Mapambano Dhidi ya Rushwa Mkoani NJombe Yamekuwa Yakikabiliwa na Changamoto Mbalimbali Ikiwemo Mtazamo Potofu wa Baadhi ya Wanajamii Kuwaona Wanaojihusisha na Rushwa kama Watu Mashujaa
Kwa Mujibu wa Taarifa ya Hali ya Rushwa Mkoani Njombe Katika Kipindi Cha Mwaka 2012 Hadi Mwaka 2013 Jumla ya Majalada 40 Yamefunguliwa na Majalada 72 ya Kesi za Rushwa Yakiendelea na Uchunguzi.
Nakembetwa Amesema katika kipindi cha mwaka jana, taasisi hiyo imeokoa kiasi cha sh. 12,642,562 kati ya sh. 85,550,797 zilizochunguzwa. Alisema kwa kipindi hicho wamefungua majarada 21, kati ya hayo 15 yanachunguzwa 6 yamefikishwa kwa DPP, huku wakifanikiwa kushinda kesi 2 na kushindwa 2, na kwamba wamefungua kesi mpya 14.