Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Article 1

$
0
0






Na Gabriel Kilamlya Njombe

Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Mkoani Njombe Imefanikiwa Kushika nafasi ya kwanza Kimkoa katika zoezi la ukimbizaji wa mbio za mwenge wa uhuru kwa mwaka 2013 Ikifuatiwa na Halmashauri ya Mji wa Njombe.

Halmashauri hiyo ya wilaya Njombe Pia Imeshika nafasi ya Tano Kwa Kanda ya Nyanda za juu kusini huku Kitaifa Ikifanikiwa Kushika Nafasi ya Tisa Katika Halmashauri zote Hapa Nchini.

Taarifa ya Ushindi Huo Imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba Wakati Akifungua kikao cha kamati ya ushauri katika Halmashauri Hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri Hiyo Ambapo Pia Mkuu Huyo wa Wilaya Ndiye mwenyekiti wa kamati ya Ushauri.

Kutokana na Ushindi huo Mkubwa kwa Halmashauri hiyo Bi.Dumba Amepongeza Jitihada kubwa zilizofanywa na wadau mbalimbali wa maendeleo katika Halmashauri hiyo kwa kuwezesha zoezi la maandalizi kwenda vizuri na kwa kasi kubwa.

Aidha Bi.Dumba Amesema Kuwa Miradi yote

Iliyowekwa Mawe ya Msingi,Kuzinduliwa na Kukaguliwa na Mwenge wa Uhuru ni lazima Ikamilike kama Alivyoagiza Kiongozi wa Mbio za mwenge huo bwana Jumma Ally Simai Ukiwa Wilayani Njombe.

Pamoja na mambo mengine amesema kuwa kukamilika kwa miradi hiyo kutatokana na uwajibikaji wa viongozi wanaosimamia miradi hiyo kwa kushirikiana na jamii nzima kiujumla ili kuendana na mpango wa matokeo makubwa ya haraka sasa[Big Results Now BRN].

Hata hivyo ameeleza kuwa watendaji wote wa Halmashauri Wanapaswa kutambua kuwa uzembe wao katika utendaji ndio uliopelekea Mawaziri Wanne Nchini Kuvuliwa Nyadhifa Zao Akiwemo Mmoja Kujiudhulu.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles