December 6, 2013, 4:18 pm
![]()
Gari aliyokuwa amepanda Katibu wa NEC,Siasa na mahusiano ya Kimataifa,Dkt Asharose Migiro ikiwa imepoteza muelekeo,kufuatia eneo hilo kukumbwa na utelezi mkubwa kutokana na mvua iliyokuwa imenyesha.Dkt.Migiro alikuwa kwenye msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana walipokuwa wakitokea Wilayani Makete kuelekea Wilaya mpya ya Wanging'ombe,mkoani Njombe mapema leo ambapo hata hivyo walifika salama na kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii. Juhudi ya kulinasua gari hilo zikiendelea kufanyika.Pichani Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa sambamba na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na wadau wengine wakitoka kutoa msaada wakati gari ya Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa iliponasa kwenye tope. Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt.Asharose Migiro akiwa amesimama kando kando ya barabara akisubiri gari yake iliyokuwa kwenye msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana,iondolewa mara baada ya kunasa kwenye tope,kufuatia eneo hilo kuharibika kutokana na mvua kunyesha na kusababisha utelezi mkubwa eneo hilo. Juhudi za kulinasua gari hilo zikiendeleA
Eneo linavyoonekanaKWA HISANI YA michuziblog
↧