YAICHAKAZA 4-2 LUPONDE FC.![]()
Hiki ni Kikosi cha Timu ya Njombe Ambayo Leo Katika Dimba la Sabasaba Mjini Njombe Kimeichakaza Timu ya Luponde FCBaada ya Kupigwa Mfululizo na Vilabu Vya Chai Fc na Makambako United Hivi Karibuni Kikosi cha Njombe Mji leo Kimemalizia HASIRA Zake Kwa Kuitandika Luponde FC Magori4-2 Leo Katika Dimba la Sabasaba Mjini Njombe
Mechi Hiyo ya Round ya Kwanza Ligi ya Taifa Ngazi Ya Mkoa Imepigwa Huku Mashabiki wakiwa na Tension Kubwa Katika Kuhakikisha Timu yao Inashinda na Kupanda na Kuwa Nafasi ya 2 Kwa Pointi 18 Toka nafasi ya Tatu Baada ya Kuchakazwa na Makambako United.
Katika Ligi Hiyo Chai Fc Bado Inashika Nafasi ya Kwanza Kwa Pointi 23 Baada ya Kumburuza Stendi Fc ya Njombe Gori Moja Bila Soka Lililopigwa Katika Dimba la
Itambo Chai Leo.
Nafasi ya Tatu Inashikwa na Makambako United Toka nafasi ya Pili Baada ya Kulazimisha Sare ya Bila Kufungana na Mbeya Road Leo.